NA GODFREY NNKO
KATIBU Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA),Prof. Said A.Mohamed leo Januari 10,2026 ametangaza matokeo ya ya upimaji wa Kitaifa wa darasa la Nne ambao ulifanyika Oktoba 22 na 23,2025 na Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili ambao ulifanyika Novemba 10 hadi 19,2025.
TAZAMA VIDEO CHINI KWA TAARIFA ZAIDI
Prof.Mohamed amesema, baraza limeidhinisha rasmi kutolewa kwa matokeo hayo ambapo upande wa usajili na mahudhurio jumla ya wanafunzi 1,583,686 walisajiliwa kufanya upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne wakiwemo wasichana 818,673 sawa na asilimia 52 na wavulana 706,513 sawa na asilimia 48.
Aidha, kwa upande wa mahudhurio kwa wanafunzi wa Darasa la Nne, Katibu Mtendaji wa NECTA amesema walikuwa asilimia 94 sawa na wanafunzi 1,490,377 katika shule za msingi 20,508.Pia, amesema wapo wanafunzi 93,309 sawa na asilimia sita ambao hawakufanya mtihani huo, licha ya kusajiliwa.
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA
STANDARD FOUR NATIONAL ASSESSMENT (SFNA) - 2025 RESULTS
MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2025
Bonyeza hapa chini kwenye mkoa wako na uchagueKwa upimaji wa Kiraifa wa Kidato cha Pili, Profesa Mohamed amesema kuwa,wanafunzi 889,264 walisajiliwa wakiwmo wasichana 492856 sawa na asilimia 55 na wavulana 396408 sawa na asilimia 45 ambapo mahudhurio yalikuwa asilimia 91.3 sawa na wanafunzi 811,575 katika shule za sekondari 6223 nchini.
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA
FORM TWO NATIONAL ASSESSMENT (FTNA) 2025 RESULTS ENQUIRIES
CLICK ANY LETTER BELOW TO FILTER CENTRES BY ALPHABET |