Hatua kubwa ya mageuzi ya kodi nchini imefikiwa kufuatia tangazo la kuanza kutumika kwa mfumo mpya wa ukusanyaji wa kodi za ndani, hatua inayotarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya mapato ya Serikali.
Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),CPA Yusuph Mwenda, amesema mfumo huo utaanza rasmi kutumika Februari 9, 2026, baada ya Serikali kuwekeza zaidi ya shilingi bilioni 100 katika ujenzi na uboreshaji wa mifumo ya kisasa ya ukusanyaji wa kodi.
CPA Mwenda amesema mfumo huo umeundwa kwa kuzingatia changamoto na malalamiko ya muda mrefu yaliyokuwa yakikabili walipa kodi, hususan katika masuala ya urahisi wa ulipaji, ufanisi wa huduma na uwazi katika makadirio na ukusanyaji wa kodi za ndani.
Ameeleza kuwa kupitia mfumo huo mpya, TRA inalenga kuongeza uwazi na uwajibikaji, kupunguza mwingiliano wa moja kwa moja kati ya mlipa kodi na mtumishi wa umma, pamoja na kuimarisha matumizi ya teknolojia katika kusimamia mapato ya Serikali.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo






















