Rais Dkt.Mwinyi atoa maagizo kwa wakuu wa mikoa aliowaapisha

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka wakuu wa mikoa wapya wa Zanzibar kuwa na utaratibu maalum unaotambulika wa kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzitafutia ufumbuzi, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Rais Dkt.Mwinyi ametoa ushauri huo leo Desemba 3, 2020 Ikulu jijini Zanzibar katika hafla ya kuwaapisha wakuu wa mikoa wapya, watakaohudumu katika mikoa mitano ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja aliyemteua hivi karibuni, Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo Desemba 3,2020. (Picha zote na Ikulu).
 
 
Walioapishwa ni Ayoub Mohamed Mahamoud wa Mkoa Kaskazini Unguja, Rashid Hadid Rashid wa Kusini Unguja, Idrissa Kitwana Mustafa wa Mjini Magharibi, Salama Mbarouk Khatib wa Kaskazini Pemba pamoja na Mattar Zahor Masoud wa Mkoa wa Kusini Pemba.

Amesema, viongozi hao wana jukumu la kuandaa utaratibu maalum utaowawezesha wananchi kuwasilisha kero mbalimbali zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi wa haraka, huku akiwataka kutokuwa sehemu ya kero hizo kwa kigezo kuwa wapo baadhi ya viongozi wanaojihusisha katika migogoro mbalimbali ikiwemo ya ardhi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Omar Othman Makungu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora, Mhe.Haroun Ali Suleiman na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mhe.Masoud Ali Mohammed, wakifuatilia hafla ya kuapishwa kwa wakuu wa mikoa walioteuliwa hivi karibuni, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakifuatilia hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa wapya,hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo Desemba 3, 2020.

Aidha, amewataka viongozi hao kuondokana na utamaduni wa kuoneana aibu au muhali, pamoja na kuwataka kusimamia kikamilifu miradi ya maendeleo iliyopo katika mikoa yao hata kama miradi hiyo inatekelezwa na wizara za Serikali.

“Mradi wowote unaofanyika katika mkoa wako ni mradi wako una jukumu la kufuatilia hata kama unatekelezwa na wizara,"amesema Rais Mwinyi.

Amesema, viongozi hao wana jukumu la kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa viwango vinavyokubalika na kumalizika kwa wakati, akibainisha kuwepo miradi kadhaa ikiwemo wa ZUSP (unaogharimu dola dola milioni 93) ambao utekelezaji wake hauridhishi kwa msingi kuwa umetekelezwa chini ya viwango katika maeneo mbalimbali.

Dkt.Mwinyi amewataka wakuu hao wa mikoa kujiridhisha iwapo miradi inayotekelezwa katika mikoa yao inaendana na thamani halisi ya fedha zilizotumika.
Wakuu wa wilaya na wanafamilia wakifuatila hafla ya kuapishwa kwa wakuu wa mikoa wa Zanzibar katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar wakiapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) hafla hiyo imefanyika leo Desemba 3, 2020. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba aliyemteua hivi karibuni, Mhe.Mattar Zahor Masoud, hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba aliyemteua hivi karibu, Mhe.Mattar Zahor Masoud, hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba aliyemteua hivi karibuni, Mhe Salama Mbarouk Khatib, hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja aliyemteua hivi karibuni, Mhe Idrisa Kitwana Mustafa, hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba aliyemteua hivi karibuni, Mhe Salama Mbarouk Khatib, hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja aliyemteua hivi karibuni, Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa, hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika leo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja aliyemteua hivi karibuni, Mhe. Rashid Hadidu Rashid, hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika leo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja aliyemteua hivi karibuni, Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud, hafla hiyo imefanyika leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi akihutubia baada ya kumaliza kuwaapisha wakuu wa mikoa wa Zanzibar katika hafla iliofanyika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi akihutubia baada ya kumaliza kuwaapisha wakuu wa mikoa wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo.

Sambamba na hayo, amewataka viongozi hao kuzifuatilia kwa karibu Manispaa na halmashauri zilizopo mikoani mwao kutokana na utendaji wa kazi usioridhisha, kiasi cha kushindwa hata kukusanya taka pamoja na kusimamia makusanyo ya fedha.

Aidha, amesema pamoja na kuwepo miradi ya wizara katika mikoa yao, wana jukumu la kubuni miradi mipya ili kutekeleza kwa vitendo ilani ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na kumtaka kila mmoja kuwa sehemu ya utekelezaji kwa vitendo ahadi alizozitoa kwa wananchi wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita.

Akigusia suala la uwajibikaji kwa watendaji, Rais Dkt. Mwinyi amewakumbusha viongozi hao wajibu walionao katika kuwasimamia wafanyakazi wao ili kila mmoja aweze kutekeleza wajibu wake na kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa wananchi, akibainisha kuwepo dhuluma,manyanyaso na udhalilishaji kwa wananchi.

Vile vile ametaka kuwepo mifumo bora ya ukusanyaji mapato ili yaweze kutatua matatizo mbalimbali katika sehemu zinazohusika, sambamba na kuwataka kuwa wabunifu, kuondokana na urasimu na kusisitiza umuhimu wa kusimamia vyema dhamana zao katika taasisi zote za ukusanyaji mapato.
Wakuu wa mikoa wapya wa Zanzibar wakifuatili kwa makini hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia baada ya kumaliza kuwaapisha katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo.
Wa kwanza kutoka kushoto ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Zuberi Ali Maulid, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe.Dkt. Mwinyi Talib Haji na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa wa Zanzibar aliowateua hivi karibuni, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Wakuu wa mikoa wapya wa Zanzibar wakifuatili kwa makini hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia baada ya kumaliza kuwaapisha katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo.
Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakifuatilia hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa wapya,hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja aliyemteua hivi karibuni, Mhe. Rashid Hadidu Rashid, hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika leo Desemba 3, 2020 katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar. (Picha na Ikulu). 

Katika hatua nyingine, Dkt.Mwinyi amewataka viongozi hao kupiga vita rushwa na kuondoa ubadhirifu katika matumizi ya mali za serikali, sambamba na kuondoa wizi katika maeneo mbalimbali , huku akisema makusanyo na fedha za bajeti zimekuwa zikipotea sana.

Aidha, amesema kuna changamoto kubwa katika suala la utiaji saini mikataba ya miradi mbalimbali nchini, ikiwemo ile ya wizara za Serikali ambapo Wizara ya Fedha imekuwa ikihodhi jukumu hilo.

Amesema, hakuna ulazima kwa wizara hiyo kuingia mkataba katika kila mradi wa wizara, akibainisha hatua hiyo inaviza utendaji kutokana na ufuatiliaji duni, akitolea mfano wa mradi wa mashine ya MRI katika Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja iliyoshindwa kutengenezwa kwa wakati kwa vile mkataba wake ulisainiwa na Wizara ya Fedha.

“Inatia mashaka kila mradi mkataba wake lazima uingizwe na Wizara Fedha,”amesema.Akiahidi kufuatilia utendaji wa wakuu hao wa mikoa hao, Dkt.Mwinyi aliwataka kufanya kazi kwa utaratibu mpya wa ubunifu na utatuzi wa kero za wananchi ili kila senti ya serikali iweze kutumika vizuri. 

Mapema, Dkt.Mwinyi amewakumbusha viongozi hao jukumu linakowakabili katika kusimamia mikoa kuwa sio jambo dogo, hivyo akawataka kutekeleza wajibu huo kwa kujituma ili kutekeleza vyema Ilani ya CCM pamoja na kuondoa kero mbalimbali za wananchi.

Aidha, amewashauri wasichelewe kujifunza majukumu yao na kufanya kazi zinazowakabili, akitaka kuweka kipaumbele suala la ulinzi na usalama kwa ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama.

Amewataka kusimamia kikamilifu Manispaa na hamashauri ziliopo mikoani mwao, akibainisha kuwepo mapungufu makubwa katika usimamizi.

Nao wakuu wa mikoa mitano ya Zanzibar, walisema wameajianda kutekeleza kikamilifu majukumu yote ya kazi zao, ili kufikia malengo yaliokusudiwa.

Viongozi mbalimbali wa kitaifa wamehudhuria katioka hafla hiyo, akiwemo Makamu wa Pili wa Rais, Hemed Suleiman Abdalla, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Abdulahamid Yahya Mzee, Mawaziri, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Dkt.Mwinyi Talib Haji, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid,Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab, Viongozi wa Idara maalum za Serikali ya Zanzibar pamoja wanafamilia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news