Mwenyekiti wa DRFA azipiga tafu timu zitakazoshiriki Mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa mikoa

Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Dar Es Salaam (DRFA), Lameck Nyambaya ametoa msaada kwa timu tatu za mkoa huo zinazoenda kushiriki Mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa yanayotarajiwa kuanza Machi 4, mwaka huu, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Nyambaya amekabidhi jezi seti moja kwa kila timu, mipira mitatu kwa kila kitu pamoja na fedha taslimu shilingi laki tatu.

Timu hizo ni Mabomba FC itakayokua kituo cha Lindi, Huduma SC itakayokua kituo cha Arusha pamoja na Temeke Squad ambayo itakua kituo cha Pwani.

Post a Comment

0 Comments