Rais Samia ampendekeza Dkt.Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amempendekeza Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isidory Mpango kuwa Makamu wa Rais, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.

Jina la Dkt.Mpango limesomwa leo Machi 30, 2021 bungeni jijini Dodoma na Spika Job Ndugai aliyeletewa bahasha yenye jina hilo na mpambe wa Rais.

Aidha, jina la Dkt. Mpango liliwekwa katika bahasha mbili ya juu ilikuwa ya kaki na ya ndani ilikuwa nyeupe, Spika Ndugai alianza kusoma nyaraka hiyo ya rais akirudia rudia maneno ya utangulizi kabla ya kulisoma jina huku baadae akisababisha shangwe kubwa bungeni baada ya kulisoma jina hilo.

KUHUSU DKT. PHILIP ISIDORY MPANGO

Dkt. Philip Mpango ni Waziri wa Fedha na Mipango katika Serikali ya Awamu ya Tano, ameteuliwa katika baraza la mwanzo la mawaziri la aliyekuwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Rais Dkt.John Magufuli. Alianza kwa ubunge wa kuteuliwa na baadae mwaka 2020 aliwania Ubunge Jimbo la Buhigwe na mkoani Kigoma na kupata ushindi wa kishindo.

Waziri Dkt.Mpango ni mzaliwa wa Kigoma, baba yake ni marehemu Isidori Nzabhayanga Mpango, ambaye alizaliwa Kijiji cha Kasumo, Wilaya ya Kasulu. 
 
Dkt.Mpango alizaliwa hapo hapo Kasumo na ni kaka mdogo wa Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanganyika Magharibi-Kasulu mkoani Kigoma, Dkt. Gerard Mpango.

Dkt. Mpango ni mchumi mwenye shahada ya uzamivu ya uchumi.Kuanzia miaka ya 1990 hadi 2000, alifanya kazi akiwa mhadhiri mwandamizi wa uchumi katika kitivo cha Biashara (sasa Shule ya Biashara) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Alikuwa akifundisha “Microeconomics”, “Macroeconomics” (kwa mwaka wa pili) na “Public Finance” kwa mwaka wa tatu na kozi za uzamili. (Kwa tafsiri yangu, Uchumi mdogo, Uchumi mkubwa na masuala ya Fedha za umma.

Amewahi kuwa Mchumi Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Mkuu wa Kamati ya kumshauri Rais Jakaya Kikwete wakati huo kuhusu masuala ya uchumi, Katibu binafsi wa Rais anayeshughulikia masuala ya uchumi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, kabla ya kuhamishiwa Tume ya Mipango, Ofisi ya Rais. Nyadhifa hizi zote amezishika wakati wa utawala wa Kikwete.

JPM alipoingia madarakani alimteua kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na baada ya siku chache akateuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Nguvu

Kwanza, Dkt. Mpango ni kiongozi mwenye msimamo thabiti. Baadhi ya watendaji ambao wamewahi kufanya kazi chini yake kwenye ofisi ya Rais wanamuelezea kama mtu anayetaka waliomzunguka wazungumze kwa takwimu na ushahidi hasa katika masuala ya uchumi. Msimamo huo pia aliuonyesha alipokuwa mtaalamu wa Benki ya Dunia. Hakuwa mwoga kuieleza ukweli Serikali pale ambako ilikuwa haifanyi vizuri.

Mathalan, wakati wasomi wengi wa uchumi wakiwa wanapiga kelele za kuisifia Serikali juu ya ukuaji wa uchumi miaka ya mwanzoni ya 2000, Dkt. Mpango alieleza wazi kuwa lengo hilo la kukuza uchumi kwa asilimia 5.9 haliwezi kufikiwa kwa sababu katika miaka minne iliyopita, Serikali ilishindwa kulifikia.Endelea hapa

Post a Comment

0 Comments