Waziri Jafo awajibika muda mfupi baada ya hotuba ya Rais Samia


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amemuagiza Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga kuwachukulia hatua Wekahazina na Wakaguzi wa ndani ambao halmashauri zao zimepata hati chafu, anaripoti Mwandishi MWANDISHI.

Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) ya mwaka 2019/20 iliyotolewa mapema leo hii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan imebainisha kuwa Halmashauri nane zimepata Hati chafu.

Rais Samia ameelekeza kuwa, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) iwajibishwe kwa sababu inachukukua pesa nyingi huku matokeo yakiwa hayaonekani.

Rais Samia amesema, ndani ya TAMISEMI kuna ufisadi mkubwa ambapo ameagiza CAG achunguzwe akishindwa aseme Serikali ifanye kazi.

Pia ametoa maagizo kuwa, mashirika ya umma yachunguzwe kwa sababu katika takwimu za ufisadi mashirika ya umma yanaongoza kwa ubadhirifu na Serikali ipo tayari kufanya maamuzi kama CAG atashindwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news