Rais Samia: Fedha zote za Januari hadi Machi tunataka kuziona

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemuagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Dkt.Charles Kichere na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenda kupitia fedha zote zilizotoka kuanzia Januari hadi mwezi huu wa Machi ili kutoa taarifa ya kazi zilizofanya, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.

Ametoa agizo hilo leo Machi 28, 2021 Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma baada ya kupokea taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) za mwaka wa fedha 2019/20 na taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mwaka 2019/2020.

"Naomba nitoe agizo kwako CAG na Gavana wa Benki Kuu yupo hapa, naomba uende ukapitie fedha zote zilizotoka kuanzia Januari hadi mwezi huu wa Machi kwenda kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo, tunataka kuziona,"ameagiza Rais Samia.

"CAG naomba sana ulimi wako usiwe na utata, kama kuna Shirika halifanyi vizuri, tuambie halifanyi vizuri, kama Bodi haisimamii vizuri, tuambie Bodi hii haisimamii vizuri, sababu tutakaposema mapungufu ndio tutakapoweza kurekebisha na tukaweza kufanya vizuri zaidi,"ameeleza Rais Samia.

Post a Comment

0 Comments