Waziri Balozi Liberatha Mulamula, Naibu Waziri Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk waanza kazi rasmi

 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberatha Mulamula akiwasili katika Ofisi za Wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma muda mfupi baada kula kiapo cha kutumikia nafasi hiyo. Mhe. Balozi Mulamula na Naibu wake Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk wamepokelewa na Watumishi na Wakuu wa Idara na Vitengo wakiongozwa Katibu Mkuu Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberatha Mulamula akikaribishwa Wizarani muda mfupi baada ya kula kiapo cha kutumikia nafasi hiyo

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akikaribishwa Wizarani muda mfupi baada ya kula kiapo cha kutumikia nafasi hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberatha Mulamula na Naibu wake Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk wakisikiliza maelezo ya Katibu Mkuu Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge mara baada ya kuwasili Wizarani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberatha Mulamula akiongea na Watumishi na Menejimenti ya Wizara (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili Wizarani
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberatha Mulamula akisaini kitabu cha wageni alipowasili Wizarani
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisaini kitabu cha wageni alipowasili Wizarani
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberatha Mulamula na Naibu wake Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi, Menejimenti na Viongozi wa Wizara mara baada ya mapokezi ya kuwakaribisha Wizarani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberatha Mulamula na Naibu wake Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi, Menejimenti na Viongozi wa Wizara mara baada ya mapokezi ya kuwakaribisha Wizarani.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Nje).

Post a Comment

0 Comments