Chelsea watwaa ubingwa Ligi Kuu England

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Chelsea imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuitandika bao 1-0 Mabingwa wa Ligi Kuu England Manchester City.
Ni katika fainali ya kukata na shoka iliyopigwa Mei 29, 2021 katika dimba la Stadio do Dragao jijini Porto, Ureno.

Bao hilo pekee kwenye mchezo huo limefungwa na kiungo mshambuliaji wa Kijerumani , Kai Havertz akimalizia pasi nzuri kutoka kwa Mason Mount lililodumu muda wote.

Wachambuzi wa soka wanasema kuwa, ubingwa wa Chelsea umeletwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya benchi la ufundi kutoka timu kuwa chini ya kocha Frank Lampard na sasa Thomas Tuchel.

Tuchel anaelezwa kuwa, kwa kiwango kikubwa ameyeonyesha uhai mpaka msimu unamalizika akiwa na nafasi ya kucheza michuano ya Ulaya pamoja na ubingwa huu.

Awali, Chelsea walikuwa hawapigiwi upatoukubeba taji la Ulaya kuanzia mwanzoni hata ilipobainika kuwa watacheza na Man City fainali bado, nafasi kubwa ilikuwa inaenda kwa Pep Guardiola na kikosi chake.

Kutokana na ushindi huo, Tuchel amewashangaza wapenzi wa kandanda kwa kuendelea mtangulizi wa mawazo ya Pep Guardiola ukiwa ni mchezo wa tatu kufungwa msimu huu baada ya nusu fainali ya Kombe la FA, Ligi Kuu England na sasa mchezo muhimu wa Uefa.

Huu unakuwa ubingwa wa kwanza kwa kocha, Thomas Tuchel, na zaidi ya asilimia 90 ya wachezaji wa kikosi cha Chelsea pia ni ubingwa wao wa kwanza.

Pia hili linakuwa taji la pili tu la Ligi ya Mabingwa kwa The Blues baada ya lile walilolitwaa msimu wa 2011–2012 wakiwafunga wenyeji, Bayern Munich katika fainali Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich, Ujerumani kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 1-1 chini ya kocha wa muda, Mtaliano Roberto Di Matteo.

Hata hivyo, ushindi huu ni mwendelezo wa ubabe wa kocha Mjerumani, Thomas Tuchel kwa kocha Mspaniola wa mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Pep Guardiola baada ya kuifunga pia Man City 1-0 kwenye Nusu Fainali ya Kombe la FA Aprili 17 na 2-1 kwenye ligi Mei 8.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news