Dkt.Mkamilo awapa neno wataalamu wa manunuzi, wajumbe wa TARI

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Dkt. Geoffrey S. Mkamilo amewataka wataalamu wa manunuzi kutoka vituo nane vya utafiti pamoja na wajumbe wa bodi ya zabuni na kitengo cha manunuzi cha makao makuu kutumia mafunzo ya sheria na kanuni za manunuzi ya umma kutenda kazi kwa ufanisi, ANARIPOTI JUNIOR MWEMEZI (TARI).
Sambamba na kutoyumbishwa na mtu yeyote katika utekelezaji wa majukumu yao pamoja na kuepuka mambo ambayo yanaweza kusababisha zabuni kutofanyika kwa haki.

Dkt.Mkamilo ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya sheria na kanuni za manunuzi yaliyofanyika katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma. 
Kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Manunizi ya Umma (PPRA),Bw. Albert Kamunde amesema anaamini kuwa kutokana mafunzo hayo yaliyotolewa kwa siku nne anaamini yatakuwepo mabadiliko makubwa ya kiutendaji katika idara hiyo. 

Naye Meneja wa Manunuzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Bw. Erick Kaswaka amesema kabla ya mafunzo hayo walikuwa wanapata utata sana katika utekelelezaji wa majukumu yao kufuatia kupewa maagizo tofauti, lakini kwa sasa kupitia mafunzo hayo kila mmoja wao atahakikisha anafanya kazi kwa kufuata sheria taratibu na kanuni za manunuzi.(PICHA ZOTE NA JUNIOR MWEMEZI-AFISA HABARI WA TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO NCHINI-TARI).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news