Kocha aliyevuruga mipango ya Simba SC Ligi ya Mabingwa Afrika atimuliwa kazi

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Siku chache baada ya kuiwezesha klabu ya Kaizer Chiefs kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika uongozi wa klabu hiyo umemfuta kazi kocha wake, Gavin Hunt.

Hunt ndiye aliyekuwa kocha mkuu wa Kaizer Chiefs (Amakhosi) wakati ikiisukuma nje ya mashindano hayo Simba SC kwa jumla ya mabao 4-3 katika hatua ya robo fainali.Tazama kilichowakuta Simba SC hapa.

Makocha wasaidizi Arthur Zwane na Dillon Sheppard watachukua nafasi yake, wakati klabu ikiendelea na mchakato wa kumtafuta mrithi wa Hunt.
"Kaizer Chiefs imemaliza mkataba na kocha Gavin Hunt. Kwa muda, Makocha Wasaidizi Arthur Zwane na Dillon Sheppard watasimamia timu. Klabu itatoa taarifa zaidi kwa wakati ujao, ”imeeleza sehemu ya taarifa kutoka kwa klabu iliyobandikwa Twitter.

Kaizer Chiefs, kupitia kocha wake Gavin Hunt, ndiye aliyezima ndoto za mashabiki wa Simba na wadau wa soka Tanzania na Afrika Mashariki kusonga mbele katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuwazidi kete Wekundu wa Msimbazi wakiwa dimbani.

Matokeo ya Kaizer Chiefs, yaliwakatisha tamamaa wadau baada ya Simba SC kushindwa kuifunga magoli matano ili kuweza kusonga mbele katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ingawa nao Kaizer Chiefs walitolewa baadaye.

Simba FC ambao walikuwa wenyeji wa Kaizer Chiefs katika Dimba la Benjamin Mkapa mkoani Dar es Salaam walionyesha mchezo wa kasi na kufanikiwa kufunga mabao matatu, lakini haikutosha kuiwezesha kusonga mbele. Kwani, tayari huko Afrika Kusini walikuwa wamefungwa mabao manne kwa sufuri.

Post a Comment

0 Comments