BREAKING NEWS:Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Dkt. Anna Elisha Mghwira afariki

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Dkt. Anna Elisha Mghwira amefariki dunia leo wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mount Meru, Arusha, ndugu wa familia wamethibitisha.

Anna Elisha Mghwira alizaliwa Januari 23, 1959 katika Hospitali ya Mkoa wa Singida akiwa ni mwenyeji wa Kitongoji cha Irao Kata ya Mungumaji iliyopo Manispaa ya Singida Mjini.
Alijiunga na shule ya msingi ya Nyerere katika miaka ya 1968- 1974. Kisha akasoma shule ya Sekondari Ihanja kutoka 1975 hadi 1978 kabla ya kujiunga na Seminari ya Kilutheri kwa masomo ya A-level 1979 hadi 1981.

Bi.Mghwira alipata shahada yake ya kwanza katika theolojia Chuo Kikuu cha Tumaini kabla ya Kujiunga Chuo Kikuu cha Dar es Es Salaam alipoongeza shahada ya sheria (LLB) mwaka 1986.

Mwaka 2000 alijiunga na Chuo Kiuu cha Essex huko Uingereza aliendelea kusoma shahada ya uzamili ya sheria (LLM).

Wakati wa uhai wake, Mghwira alifanya kazi katika mashirika ya kimataifa na ya Kitanzania yanayoshughulikia uwezeshaji wanawake, maendeleo ya jamii na wakimbizi. Unakumbuka huu wimbo wake?


Huyu ni kati ya watu ambao walizaliwa katika familia ya wanasiasa kwani, baba yake alikuwa diwani kupitia Chama cha TANU ambapo, yeye Anna alijiunga na umoja wa vijana wa chama hicho.

Katika miaka ya 1970 alipunguza kazi yake ya kisiasa ili aweze kuzingatia masomo yake na familia.

Mwaka 2009 alirudi katika siasa alipojiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Bi Mghwira alishikilia nyadhifa tofauti kama katibu wa wilaya wa chama na baadaye mwenyekiti wa wilaya wa chama.

Aidha,mwaka wa 2012, alishindwa na Joshua Nassari katika uteuzi wa CHADEMA kwa uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha. Alifanikiwa kugombea kiti cha Bunge la Afrika Mashariki mwaka huo huo ingawa kura hazikutosha

Machi 2015, alihama CHADEMA kwenda chama kipya cha ACT WAZALENDO ambapo baadaye aliteuliwa kuwa mwenyekiti taifa wa chama wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa chama. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka huo aligombea nafasi ya urais wa Tanzania bila mafanikio.

Mwaka 2017 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akaacha ACT-Wazalendo akahamia Chama cha Mapinduzi (CCM). Uteuzi huo ulifanywa na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt.John Pombe Joseph Magufuli.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news