Polisi wakiri kumshikilia Freeman Mbowe, asafirishwa kwenda Dar

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limethibitisha kumshikilia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mheshimiwa Freeman Mbowe kwa ajili ya mahojiano.

Ramadhani Ng'anzi ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza amesema, Mheshimiwa Mbowe aliwekwa mbaroni alfajiri ya kuamkia Julai 21,2021 akiwa hoteli ya Kingdom mtaa wa Ghana jijini Mwanza.

Amesema, baada ya kumkamata, "wenzetu wa Dar es Salaam nao walitueleza kuwa wanamtafuta kwa makosa mengine anayodaiwa kuyafanya huko, hivyo tulimsafirisha kwenda Dar es Salaam anakoendelea kuhojiwa," amesema Kamanda huyo.

Post a Comment

0 Comments