Wizara ya Mawasiliano kuwajengea wataalam wake uelewa

Na Doreen Aloyce,Diramakini Blog

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainabu Chaula amefungua kikao kazi cha wataalamu wa ukaguzi wa ndani,wahasibu ili kujenga uelewa wa pamoja kuhusu namna ya kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CGA ).

Kauli hiyo ameitoa leo wakati alipokuwa akizungumza na wataalamu hao katika ukumbi wa wizara hiyo jijini Dodoma.

Amesema, kama msimamizi mkuu ameamua kuitisha kikao hicho kwa ajili ya kuwekana sawa juu ya maandalizi katika ukaguzi wa ndani na kuzifanyia kazi ili pale Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ( CAG) anapokuja kukagua akute mambo ni mazuri.

"Tumeamua wote kwa pamoja kukaa kikao kazi cha ukaguzi wa ndani na wataalamu wa fedha na taasisi zote sita ninazozisimamia ambazo zinapaswa kufuata kanuni na kuhakikisha tunapeana mikakati juu ya utendaji kazi wetu na kuangalia mafanikio poja na changamoto ukizingatia wizara hii bado ni mpya,"amesema Chaula.

Aidha, amesema wanataka kuweka maandalizi kutengeneza utamaduni wa uwajibikaji wa pamoja ili Mkaguzi akija akute mambo ni mazuri kuna mambo mengine ni ya msingi, lakini hayatekelezwi.

Nae Mkaguzi Mkuu wa Ndani kutoka wizara hiyo, Joyce Christopher alisema kuwa lengo lingine ni kuweka mipango ya pamoja,utekelezaji hoja zilizotolewa na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali na kuzifanyia kazi pamoja na kuhakikisha na kuyajadili na kuboresha ili wanapofunga mwaka kusiwe na hoja zozote.

"Tunapoelekea kufunga mwaka tumeona tukutane kujadili mambo mbalimbali ya utendaji kazi wetu na kwa kufanya kazi kwa pamoja ambapo pia tunajipanga kuweka sawa zile hoja za CAG zinafanyiwa kazi na anapokuja akute mambo ni mazuri,"amesema Christopher.

Kwa upande wake Octavian Barnabas, Mkaguzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano (TTCL) alisema kuwa, kupitia kikao hicho kinaenda kuleta tija kwani kinawasaidia kuweza kubadilishana uzoefu na kupeana ushauri juu ya utendaji kazi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news