Aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha,Basil Mramba afariki

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Basil Mramba ambaye amewahi kuwa Waziri wa Fedha katika Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Hayati Benjamin Mkapa amefariki dunia.

Kwa mujibu wa mtoto wake, Godfrey Mramba, baba yake amekutwa na umauti leo asubuhi wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Regency.
“Mzee amefariki mapema leo (Agosti 17,221), ameugua pale Regency Medical Centre muda wa wiki mbili, amepata maradhi ya Covid-19 tumempoteza leo, tunamshukuru Mungu kwa maisha yake na tutayasherehekea,”amesema.

Kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini kimetokea leo kwa ugonjwa wa Corona mkoani Dar es Salaam.

Godfrey ameweka wazi kuwa, kutokana na janga la virusi vya Corona (Uviko-19) msiba huo utahusisha watu wa familia pekee ili kuepuka mkusanyiko. Basil Mramba alizaliwa Mei 15, 1940. Uongozi wa Diramakini Blog unawapa pole ndugu, jamaa na marafiki kwa Msiba huu. Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news