Rais Dkt.Mwinyi aivunja Bodi ya Wakurugenzi ZIC, ateua viongozi mbalimbali

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameivunja Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Bima la Zanzibar(ZIC) kuanzia tarehe 18 Agosti, 2021 na kumteuwa Bwana Ramadhan Mwalim Khamis kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu jijini Zanzibar, uteuzi huo unaanzia tarehe 18 Agosti, 2021

Aidha, Mhe. Rais Dk. Mwinyi amemteua, Mhe. Balozi Amina Salum Ali kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Takwimu Zanzibar kuanzia tarehe 16 Agosti, 2021.

Mhe. Rais Dk. Mwinyi pia amefanya uteuzi wa Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu kama ifuatavyo;

1) Bibi Salma Haji Saadat ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu.

2) Bwana Ussy Khamis Debe ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu. Uteuzi huo umeanzia tarehe 18 Agosti, 2021.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news