RC Tabora atoa elimu ya chanjo ya UVIKO-19 kwa wafanyabiashara

NA TIGANYA VINCENT,RS-TABORA

WAFANYABIASHARA katika Mnada wa Ushirika ulipo Mjini Nzega washauriwa kuchangamkia chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO 19 ili waendelee kuwa salama na kuendesha shughuli zao za kujiingizia kipato halali.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dkt. Batilda Buriani wakati wa ziara yake inayoendelea ya utoaji wa elimu umuhimu wa chanjo ya UVIKO 19 katika maeneo mbalimbali za Mkoa huo.

Amesema, afya ni mtaji muhimu kwa kila mwanadamu na pindi anapokuwa mgonjwa shughuli zake zinateteleka na kurudisha nyuma maendeleo yake.

Balozi Dkt. Batilda Buriani amesema, chanjo ya UVIKO-19 ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameileta ni salama na muhimu katika kulinda afya za wananchi na kuwawezesha kuchapa kazi bila matatizo.

Amesema Rais Samia anawapenda wananchi wake na ndio maana ameamua kuwatafutia chanjo dhidi ya ugonjwa hatari wa UVIKO-19 ambao umeshapoteza nguvu kazi na kuzorotesha uchumi wa dunia.

Balozi Dkt. Batilda alisema kuwa watu waliochanja wako katika mazingira mazuri ya kutopoteza maisha hata kama wakipata maambukizi ya UVIKO 19 , lakini wale ambao hawachanji wako kwenye uwezekano mkubwa wa kupoteza maisha pindi watakapopatwa na ugonjwa huo.

Mkuu huyo wa Mkoa amewaagiza watendaji katika sekta ya Afya kusogeza huduma za chanjo ya kujikinga na UVIKO 19 karibu na maeneo ambayo watu wengi wanaendesha shughuli zao za kujitafutia ridhiki.

Amesema, umbali wakati mwingine umechangia baadhi ya wananchi kutoshiriki zoezi hilo la chanjo.

Baadhi ya wafanyabiashara katika mnada huo wameishukuru Serikali ya Mkoa wa Tabora kwa kuwapa elimu kuhusu chanjo kwa kuwa hapo awali walikuwa hawana elimu sahihi jambo lililowafanywa kuchelewa kuchanja.

Walisema baada ya kudhibitishwa na Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora kuwa Rais Samia amechanja na viongozi mbalimbali wamechanja na chanjo ni salama wako tayari na kupata chanjo hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news