Mamia wajumuika katika maziko ya baba yake Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

NA MWANDISHI MAALUM

MWILI wa marehemu baba yake Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe.Hussein Bashe, Sheikh Mohamed Bashe umepumzishwa usiku wa Novemba 24, 2021 katika Makaburi ya Waislamu Kitongo Mjini Nzega mkoani Tabora.
Akizungumza kwa niaba ya familia, Mhe. Bashe amesema familia inashukuru mchango wa jamii ya wakazi wa Nzega kwa namna walivyojitokeza kushiriki na familia katika mazishi hadi maziko ya baba yake.

Kabla ya mazishi ilifanyika ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Sheikh Bashe iliyoswaliwa katika Msikiti wa Ijumaa mjini Nzega huku ikuwakutanisha mamia ya wananchi.Marehemu Sheikh Mohamed Bashe alifariki Novemba 23, 2021 nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu.

Post a Comment

0 Comments