'Tunakemea unajisi na wizi wa mabaki ya Heri Kijangwa'

VANCOUVER (CANADA)-Tarehe 26 Oktoba 2021, kaburi la marehemu, Heri Shekigenda Kijangwa, ambaye aliishi na ualbino, pamoja na kuwa mmoja wa wanufaika wa programu yetu ya elimu, lilinajisiwa katika kijiji cha Tanda, Lushoto wilaya ya Tanga, Tanzania. 

Wahusika walichimba kaburi lake na kuiba jeneza lenye mabaki yake. Wahusika wabaki huru, na jeneza wala mabaki yake hayajapatikana.
Heri alifariki mwaka jana, Julai 4, 2020 kutokana na saratani ya Ngozi, akiwa na umri wa miaka 45, na kuzikwa Julai 7, 2020. 

Wakati wa kifo chake, Heri alikuwa msimamizi wa maabara hospitali ya Temeke. Pia alikuwa anakamilisha shahada ya pili, ya afya kutoka Chuo Kikuu cha Muhimbili. 

Awali ya hapo, alitimiza Shahada ya Sayansi katika Chuo cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia, alichohitimu mwaka 2015. Shahada zote zilifadhiliwa na programu yetu ya Elimu. Heri ameacha mke na watoto wadogo, wanne. 

Tunawapa pole familia ya Heri ambao wameathirika na uhalifu huu, mda mfupi baada ya kumpoteza Heri kwa saratani ya ngozi.

Tunalaani kwa ukali uhalifu huu na kila upungufu na uvumilivu upande wa serikali, pamoja na ubaguzi unaojidhihirisha katika jamii kwa ujumla ambao unawezesha mahalifu kama haya, nchini. 

Tunatoa wito kwa serikali ya Tanzania kuongeza jitihada zake katika kuzuia saratani ya ngozi. Pia tunaitaka serikali kuharakisha juhudi zake za uchunguzi na kuwafungulia mashtaka wahusika wa uhalifu huu.

Under The Same Sun (UTSS) imekuwa mstari wa mbele kutetea haki za watu wenye
ualbino kimataifa – hasa Tanzania na Afrika, tangu ilipoanzishwa mwaka 2008. UTSS
ina hadhi ya uangalizi katika Umoja wa Kiafrika na Umoja wa Kimataifa. Na pia, inaongoza Mtandao wa Ualbino wa Kiafrika.

Post a Comment

0 Comments