Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Bagamoyo atangaza nafasi ya kazi

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Shauri Selenda ametangaza nafasi ya kazi kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira nafasi moja.
Bagamoyo ni miongoni mwa miji yenye vivutio mbalimbali vya utalii yakiwemo majengo mazuri ya kale. (Picha na Mtandao).

Kwa mujibu wa Shauri kila mwenye sifa ya kujaza nafasi hiyo anakaribishwa kwa ajili ya kuwasilisha maombi yake.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji huyo, muombaji katika nafasi hiyo, anatakiwa kuwa na elimu ya Kidato cha Nne au Sita na awe na Shahada ya Utawala au Sheria katika moja wapo ya fani za Utawala wa Umma au Sheria.

Pia anapaswa awe na uzoefu usiopungua miaka 10 katika masuala ya Utawala na Sheria, taratibu zingine endelea kusoma hapa chini; 

Post a Comment

0 Comments