Ruvu Shooting yaingia kandarasi na wachezaji saba

NA MWANDISHI DIRAMAKINI 

UONGOZI wa Timu ya Ruvu Shooting ya Pwani umeimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji saba wapya.
Usajili huo unalenga kuongeza nguvu kuelekea sehemu iliyobaki ya Ligi Kuu ya NBC.

Waliopewa kandarasi ni Benedict Tinocco, beki Iddi Mfaume Mobby kutoka Geita Gold, winga Haroun Chanongo na mshambuliaji Abalkassim Suleiman kutoka Mtibwa Sugar. 

Pia wapo kiungo Hussein Suleiman (Chuse) kutoka Mbao FC ya Mwanza, beki Jaffar Mohamed kutoka Namungo FC na mshambuliaji Hamad Rajab Majimengi kutoka Coastal Union.

Post a Comment

0 Comments