TANZIA:Mwanahabari na msanii maarufu nchini Mzee Barnabas Maro afariki

NA MWANDISHI DIRAMAKINI 

MWANAHABARI mkongwe na mmoja wa wasanii maarufu nchini, Mzee Barnabas Maro maarufu katika tasnia ya michezo ya kuigiza na filamu kwa majina ya Mzee Kambaulaya au Baba Bishanga amefariki dunia.
Mzee huyo amefikwa na umauti usiku wa kuamkia leo Januari 4,2022 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu. 

Kwa mujibu wa taarifa za awali, msiba uko nyumbani kwake Kipunguni njia ya kuelekea Kitunda, Dar es Salaam. 

Uongozi wa DIRAMAKINI BLOG unawapa pole ndugu, jamaa na marafiki kwa kuondokewa na mpendwa wao Mzee Maro.

Mwenyenzi Mungu ailaze roho ya baba yetu mpendwa, rafiki mwema na mpenda watu mahali pema. Amen

Post a Comment

0 Comments