Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi leo

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua Balozi Hammed Mwinyi Mzale kuwa Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Februari 18, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi wa Balozi Mzale unaanza leo Februari 18, 2022.

Post a Comment

0 Comments