Rais Samia ateua viongozi wapya akiwemo bosi wa MSD

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amemfuta kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD).
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku chache baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kubaini bohari hiyo ilishikilia zaidi ya shilingi Bilioni 14 za hospitali kwa mwaka mzima bila kupeleka madawa na vifaa tiba.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi. Zuhura Yunus jijini Washington DC nchini Marekani, Rais Samia amemteua Afisa Mwandamizi katika Kampuni ya PricewaterhouseCoopers (PwC), Bi. Rosemary Slaa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bohari ya Dawa.

Pia amemteua Kiongozi Mkuu wa Mradi wa USAID Global Health Supply Chain Technical Assistance, Bw. Mavere Tukai kuwa Mtendaji Mkuu wa MSD.

Post a Comment

0 Comments