Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, wenzake wanusurika kifo katika ajali

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, Basila Mwanukuzi amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, Bombo baada ya kupata ajali ya gari.
Ni ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo eneo la Hale lililopo Korogwe katika Barabara ya Tanga-Segera.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, David Mwasimbo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Amesema,ajali imetokea usiku wa kuamkia leo, "Mkuu wa Wilaya anaendelea vizuri isipokuwa dereva wake hali si nzuri, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi, dereva alikuwa anajaribu kuyapita magari mengine na ndipo ajali ikatokea,"amesema Kaimu Kamanda huyo.

Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo, Dkt. Jonathan Gudemo amekiri kuwapokea majeruhi watatu wa ajali hiyo akiwemo mkuu huyo wa wilaya.

Dkt.Gudemo amesema, majeruhi wawili hali zao zinaendelea kuimarika akiwemo Mkuu wa Wilaya na bado wapo chini ya uangalizi wa matabibu.
"Majeruhi mmoja tumempatia rufaa ya kwenda Muhimbili (Hospitali ya Taifa Muhimbili) kwa ajili ya matibabu zaidi,amesema Dkt.Gudemo.

Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani mara kwa mara wamekuwa wakisisitiza kuhusu umuhimu wa kuzingatia kanuni, tararibu na sheria za usalama barabarani.

Pia wamekuwa wakiwataka madereva bila kujali wanaoendesha viongozi kuepuka mwendokasi kwa kuwa ni moja ya chanzo cha ajali za mara kwa mara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news