Simba SC yashindwa kuonesha makali kwa Azam FC, yatoa nafasi nzuri kwa Yanga

NA DIRAMAKINI

WEKUNDU wa Msimbazi Simba SC wamefikisha alama 50 huku wakiwa nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara yenye jumla ya timu 16 huku watani zao Yanga SC wakiendelea kuwa kileleni kwa alama 60.
Leo Mei 18,2022 Simba SC wameshindwa kuonesha makali yao, baada ya Wana Lambalamba Azam FC kuwalazimisha sare ya bao 1-0.

Ni kupitia mtanange ambao umepigwa katika Dimba la Azam Complex lililopo Kata ya Chamanzi katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Katika mtanange huo, Azam FC walitangulia na bao la mshambuliaji Mzambia, Rodgers Kola dakika ya 37 akimalizia pasi ya chipukizi Sospeter Bajana.

Ni kabla ya Nahodha John Raphael Bocco kuisawazishia Simba SC akiifunga timu yake ya zamani dakika ya 44 kwa pasi ya Shomari Kapombe.

Aidha, Azam FC baada ya sare ya leo inafikishaalama 33, ingawa inabaki nafasi ya tano ikizidiwa alama moja na Geita Gold na alama tatu na Namungo FC baada ya wote kucheza mechi 24.

Timu mbili za kwanza zitacheza Ligi ya Mabingwa na mshindi wa tatu atacheza Kombe la Shirikisho Afrika.

Lakini bingwa wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) atatokana na timu tatu za juu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news