SIKU moja baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutangaza majina ya wateule ambao watapeperusha bendera ya chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, mwaka huu, joto limezidi kupanda kwa wanachama ambao hawakukidhi vigezo.
Kutokana na hatua hiyo, leo Agosti 21, 2020, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tunduru (na baadaye Tunduru Kusini) kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM (2007-2015), Mtutura Abdallah Mtutura amehama CCM na kujiunga na ACT Wazalendo, anaripoti Mwandishi Wetu...
Mtutura amekabidhiwa kadi ya ACT Wazalendo na Katibu Mkuu wa
ACT Wazalendo, Ado Shaibu katika Ofisi ya ACT Wazalendo Tunduru mkoani Ruvuma. Kwa kina zaidi, ungana nasi kupitia www.diramakini.co.tz taarifa kamili zitakujia punde
Tags
Siasa
