Pia wenyeviti wa Kitaifa watatu wa vyama vya siasa akiwemo Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ataunguruma Jimbo la Hai, huku Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Agustino Lyatonga Mrema wakiunguruma Jimbo la Vunjo.
WAGOMBEA wa ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika majimbo nane kati ya tisa ya uchaguzi yaliyopo Mkoa wa Kilimanjaro wamechukua fomu kuomba kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kupeperusha bendera ya chama hicho, inaripoti www.diramakini.co.tz
Waliochukua fomu hizo ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt.Charles Kimei anayegombea Jimbo la Vunjo,Profesa Adolf Mkenda Jimbo la Rombo,Profesa Patrick Ndakidemi Jimbo la Moshi Vijiji, Priscus Tarimo Jimbo la Moshi Mjini, Saashisha Mafuwe Jimbo la Hai,Joseph Thadayo Jimbo la Mwanga, Anna Kilango Jimbo la Same Mashariki na Mathayo David Mathayo Jimbo la Same Magharibi.
Wagombea hao kwa nyakati tofauti wamejitokeza katika ofisi za halmashauri kwa wasimamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua fomu hizo, na kila mmoja mbali na kushukuru kwa kuaminiwa na chama hicho, wameieleza www.diramakini kuwa, wanakwenda kupata ushindi mkubwa na wa kishindo.
Katika Mkoa wa Kilimanjaro, mbali na CCM, vyama vingine ambavyo wagombea wamejitokeza kuomba kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, katika majimbo mbalimbali,kugombea nafasi ya Ubunge ni kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ACT-Wazalendo, CUF, NCCR Mageuzi,TLP na SAU.
Pia kwenye uchaguzi huu, Kilimanjaro wenyeviti watatu wa Kitaifa wa vyama vya siasa, Ni miongoni mwa wagombea waliojitokeza kugombea ubunge mkoani Kilimanjaro, ambapo Mwenyekiti wa CHADEMA, Freemani Mbowe, ataunguruma jimbo la Hai, huku Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na Agustino Lyatonga Mrema wakiunguruma Jimbo la Vunjo.
Karibu! Tovuti hii ya www.diramakini.co.tz imesajiliwa rasmi na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kupewa leseni namba TCRA/OCS-BL/0197/2020 chini ya Diramakini Business Limited iliyosajiliwa nchini Tanzania kwa ajili ya kukuhabarisha, kukuelimisha na kukupasha habari mbalimbali toka ndani na nje ya nchi. Je? Una habari,maulizo au tangazo, unataka kutupa ufadhili? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com Asante.


