Jeshi laagizwa kukamilisha ujenzi wa Ikulu kwa wakati, Katibu Mkuu Kiongozi awapa kongole

KATIBU Mkuu Kiongozi, Mhandisi Balozi John Kijazi amemtaka Mkandarasi wa Ikulu ya Chamwino  mkoani Dodoma kuhakikisha anakamilisha mradi wa ujenzi kama ilivyopangwa, inaripoti www.diramakini.co.tz

Alitoa wito huo  wakati wa ziara ya makatibu wakuu na manaibu Katibu Wakuu  katika eneo la ujenzi wa mradi huo juzi Agosti 21, 2020.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi akitoa neno la shukrani kwa Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu kwa kutembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Ikulu Chamwino jijini Dodoma jana.
“Kazi ya ujenzi inaendelea vizuri na kasi inaridhisha hivyo ongezeni kasi zaidi ili mradi ukamilike ikiwezekana kabla ya muda uliopangwa bila kuathiri ubora wa majengo,”alisisitiza Balozi Kijazi.
Akifafanua, Balozi Kijazi alisema, Serikali imewapa JKT kazi ya ujenzi huo kwa sababu inawaamini na inaamini watatekeleleza kwa gharama nafuu ikilinganishwa na wakandarasi wengine.

Aliongeza kuwa, uamuzi wa kuwapa kazi ya ujenzi wa Ikulu ni wa kimkakati na una manufaa kwa Taifa.

Aidha, aliipongeza JKT kwa kazi nzuri mnayofanya katika kutekeleza mradi huo  na kuwataka  kila kazi ambayo mkandarasi anafanya ilenge kukamilisha kazi ya ujenzi kwa wakati uliopangwa.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Brigedia Jenerali  Rajab Mabele akizungumza wakati Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali wakiongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi walipotembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Ikulu Chamwino jijini Dodoma jana.Naye Mkurugezi Mtendaji wa SUMA JKT, Brigedia Jenerali Rajab Mabele alisema kuwa, ujenzi wa Ikulu unaendelea kwa kasi kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya JKT na TBA ambao ni wasimamizi wa mradi huo.

Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali wakiongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi jana Agosti 21, 2020 ambapo walitembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Ikulu Chamwino jijini Dodoma. Ujenzi wa Ikulu ya Chamwino unatarajiwa kukamilika Desemba, mwaka huu.

“Tunamshukuru Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuendelea kutuamini na kutupa kazi hii ya ujenzi wa Ikulu hapa Chamwino,”alisema.

Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu kutoka wizara mbalimbali wakiongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi jana Agosti 21, 2020 ambapo walitembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Ikulu Chamwino jijini Dodoma. Ujenzi wa Ikulu ya Chamwino unatarajiwa kukamilika Desemba, mwaka huu.

Akifafanua alisema kuwa, miradi iliyotolewa na wizara mbalimbali imeiwezesha SUMA JKT kununua mitambo, vifaa vya kisasa, magari na hivyo kuongeza ufanisi katika utendaji.

Aliongeza kuwa, SUMA JKT itaendelea kufanya kazi usiku na mchana kukamilisha mradi huu kwa wakati ambapo katika kutunza mazingira wamepanda miti zaidi ya 5,600 katika eneo hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news