Mgombea Ubunge ACT-Wazalendo Kigamboni asema akipewa ridhaa Oktoba 28 ataanza na haya

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Kigamboni kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo, Mwanaisha Mndeme amewaomba wananchi wa Kigamboni wamchague ili awe mbunge wa jimbo hilo huku akihaidi kulinda haki za wavuvi wilayani humo.

Amesema kuwa, ni miaka zaidi ya 10 jimbo hilo limekuwa chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),lakini hadi leo vijana wa Kigamboni karibu asilimia 79 hawana ajira rasmi.

Mwanaisha ameyasema hayo Septemba 13, mwaka huu katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika viwanja vya Tungi Mnadani Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Mgombea ubunge Kwa tiketi ya Chama cha Act Wazalendo Jimbo la Kigamboni Mwanaisha Mndeme katikati akiwa sambamba na baadhi ya wanachama wa Chama hicho mara baada ya kumpokea wakati akielekea viwanja vya Tungi Mnadani Kwa ajili ya mkutano wa hadhara wa Kampeni leo.

Amesema, endapo wananchi wa Kigamboni wakimchagua basi hatua ya kwanza ni kushughulikia changamoto za wavuvi.

"Nawaomba ndugu zangu mnichague kwani shida zenu nazijua na ni za miaka mingi sekta ya uvuvi .ukosefu wa ajira kwa vijana,mikopo kwa akina,ukosefu wa huduma bora za afya haya yote mkinichagua nitakwenda kuyashughulikia,"amesema Mwanaisha.

Ameongeza kuwa, Kigamboni kuna changamoto ya makazi bora, hivyo kama watamchagua atatumia elimu yake ya uanasheria na kushirikiana na watu wa mipango miji na mazingira kuhakikisha wanapima ardhi ili wananchi wapate fursa ya kukopesheka.

Mgombea ubunge Jimbo la Kigamboni kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Mwanaisha Mndeme akiwa na mgombea udiwani wa chama hicho Kata ya Tungi, Ally Sharif wakiomba kura mbele ya wananchi (hawapo pichani) leo wilayani Kigamboni.

\Amesema kuwa, miaka kumi ya mbunge aliyemaliza muda wake ni miaka ya changamoto nyingi kwa wananchi wa Kigamboni na ndio maana hata yeye mwenyewe anakiri huku akiwataka wananchi wamchague tena ili akamalizie kazi na kwamba wamkatae kwani hatoshi.

"Ndugu zangu mimi ni biti mdogo, lakini ni mwanasheria nawahakikishia mkinipa kura nakwenda kufanya mambo makubwa kwa ajili ya Kigamboni yetu, si mnajua changamoto za afya zilivyo madawa tatizo,lakini upande wa elimu madarasa machache katika shule zetu nitahakikisha mkinichagua tunakwenda kumaliza kero hii,"amesema.

Amefafanua kuwa, katika halmashauri kuna mikopo asilimia kumi inatoka katika makundi matatu ya vijana,akina mama na walemavu asilimia mbili, wakimchagua atakwenda kuwambania ili nawenyewe wanufaiki nayo tofauti na ilivyo sasa ambapo wachache ndio wanafaidika.


                     Mgombea Mwanaisha Mndeme.

Pia amezungumzia kuhusu soko kwamba Wilaya ya Kigamboni kwa muda mrefu imekosa soko la uhakika hali inayowalazimu wananchi kufuata huduma nje ya Kigamboni wakati maeneo ya wazi hapo hivyo wakimchagua atashughulikia kero hiyo ambayo ki kubwa Kwa wananchi hao.

Alimaliza kwa kuwaomba wananchi hao ili mambo yaende vizuri basi wahakikishe wanampa kura Diwani anayotokana na chama hicho, Ally Sharif pamoja na mgombea urais Bernard Membe ifikapo mwezi Oktaba 28, mwaka huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news