Seneta atozwa mamilioni ya fedha kwa kumdhalilisha mwanamke

Seneta Elisha Abbo. (nairametrics)

Mahakama Kuu mjini Abuja, Nigeria imemuamuru Seneta Elisha Abbo kulipa Naira milioni 50 ambazo ni zaidi ya dola 130,000 na kuagizwa amuombe msamaha mwanamke, Osimibibra Warmate aliyemtukana katika duka la kuuza vifaa vya kujifurahisha wakati wa tendo la ndoa mwaka jana.

Imeelezwa na Mahakama kuwa, kitendo kilichofanywa na Seneta Abbo kilimdhalilisha na kukiuka haki ya muathiriwa huyo.

Tukio hilo ambalo lilinaswa katika kanda ya video na kusambazwa katika mitandao ya kijamii ilimuonesha Seneta Abbo akimzaba kofi Warmate.

Baada ya kitendo hicho kulaaniwa vikali na kusababisha maandamano, Seneta huyo aliomba radhi, lakini Warmate alikuwa tayari amewasilisha kesi mahakamani.

Mbali na fedha taslimu ambazo Seneta huyo anatarjiwa kumlipa Warmate mahakama imemuagiza Seneta Abbo kumuomba radhi kupitia gazeti la kila siku la kitaifa ambapo hatua hiyo imeungwa mkono na wanaharakati wa kutetea haki za wanawake nchini humo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news