Tume yakinyima usajili chama cha siasa kinachoegemea kwenye ubaguzi,kutumia vibaya bendera ya Taifa

Tume Huru ya Uchaguzi ya Afrika ya Kusini (IEC) imekinyima usajili Chama cha Siasa cha Action SA kilichopo chini ya Bw.Herman Mashaba kutokana na kukosa sifa na kukiuka baadhi ya miiko ya usajili wa vyama vya siasa nchini humo, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Mwenyekiti wa Chama Action SA,Herman Mashaba.(AFP).

Pia chama hicho kinadaiwa kuwa na mfanano wa mambo mengi na Chama cha Party of Action (POA), na kinamtuhumu Bw.Mashaba kwa kuiba logo yao. Soma POA: Mashaba ameiba logo yetu.
Bw.Mashaba amejizolea umaarufu wakati alipokuwa Meya wa jiji la Johannesburg ambapo aliongoza mapambano ya kukomesha uhalifu na pia kuondoa wahamiaji haramu jijini humo.

Chama hicho cha Bw.Mashaba kilipata umaarufu kwa sera yake ya kuwaweka raia wazawa mbele na kushinikiza wageni waondolewe nchini Afrika ya Kusini.

Hata hivyo, Bw.Mashaba ameonesha kutokubali uamuzi huo wa tume na amesema kuwa atapambana mpaka chama hicho kipate usajili. 

Mbali na kwenda kinyume na maadili chama hicho kimekiuka taratibu kwa kutumia alama ya bendera ya Taifa hilo kwenye logo ya chama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news