Shirika la Madini la Taifa laingiza mitambo ya kisasa kufanikisha uchorongaji

SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limeingiza mitambo mitatu ya uchorongaji yenye teknolojia na ya kisasa zaidi kuwahi kutumika hapa nchini.

Mmoja kati ya mitambo hiyo una uwezo wa kuendeshwa kwa kutumia kompyuta na mtu akiwa mbali na mashine.

Tukio la uziduzi limefanyika Septemba 15, 2020 na kudhirisha kwa umma wa Tanzania kuwa, shirika limethubutu na limedhamiria kuleta mapinduzi katika soko la madini kwa kuingia kwa nguvu zote kwenye shughuli za uchorongaji.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mitambo hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila ameipongeza STAMICO kwa hatua kubwa waliofikia na uthubutu wa kuleta ushindani katika soko la uchorongaji, pia amewataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuleta tija na maendeleo kwa Taifa.

Akizungumzia kuhusu mitambo hiyo, Mkurugezi wa STAMICO, Dkt.Venance Mwasse amesema ni jambo la kujivunia sana kununua mitambo hiyo ya kisasa.

“Tumeagiza mitambo hii mitatu ya kisasa kabisa na mmoja kati ya huo mtambo ni Explorac 235 wenye uwezo wa kuchimba hadi mita 500 kwa siku.

"Mtambo huu ni mpya na teknolojia yake ni ya hali ya juu na hakuna kampuni nyingine ambayo imeshawahi kutumia mtambo kama huu hapa nchini. STAMICO ndio shirika la kwanza kuwa na mtambo kama huu,"amesema.

Dkt. Mwasse ameishukuru Wizara ya Madini kwa maelekezo na ushirikiano unaoendelea kutolewa kwa STAMICO na kutoa rai kwa wadau wa uchorongaji kufanya kazi na STAMICO.

Mitambo hiyo inategemea kusafirishwa kwenda maeneo mbalimbali tayari kuanza kazi ya uchorogaji mara moja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news