TRA kupitia Mlango kwa Mlango yawaunganisha wafanyabiashara, wananchi jijini Arusha

MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) inaendesha kampeni ya elimu kwa mlipa kodi kwa muda wa wiki moja katika Mkoa wa Arusha, lengo likiwa ni kuhamasisha umma kujua umuhimu wa kodi na kuwapa uelewa wa masuala ya kodi ili waweze kutimiza wajibu wao kisheria wa kulipa kodi kwa wakati.
Afisa Msimamizi wa Kodi Mkuu, James Ntalika kutoka Kitengo cha Elimu kwa Mlipakodi TRA makao makuu jijini Dar es Salaam na Eugeni Mkubo kutoka TRA Arusha wakitoa elimu kwa wafanyabiashara katika maeneo ya stendi ndogo mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Idd Kimanta wakati akizindua kampeni hiyo amewasisitiza TRA wahakikishe kwamba,kampeni hiyo ya elimu kwa mlipakodi inafanyika katika mkoa wote na wasikazanie mjini tu bali waende katika wilaya zote sita ndani ya mkoa,sekta zote zikiwemo za utalii,kilimo,ufugaji na wafanyabiashara wa aina zote wakiwemo wananchi.

Amesema kuwa, kodi ya mapato ina manufaa makubwa kwa nchi ambapo miradi mbalimbali imekuwa ikitekelezwa na Serikali.
Mtumishi wa TRA,Mercy Macha akiendelea kutoa elimu ya mlipakodi kwa mfanyabiashara mwenye duka namba 132 maeneo ya stendi ndogo jijini Arusha.

Pia Mkuu huyo amesema,miradi mikubwa ya kimkakati na ile ya kimaendeleo inayosimamiwa na Serikali kwa maelekezo ya Rais Dkt.John Magufuli inatokana na kodi zinazolipwa na Watanzania.

''Miradi hiyo ni kama  Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere,treni ya mwendokasi,ununuzi wa ndege kubwa za abiria,ujenzi wa miundombinu ya barabara kama vile 'flyovers' za kuunganisha mikoa,''amesema Kimata.

Mkuu huyo amesema, ukusanyaji wa kodi unafanyika nchi nzima kupitia TRA,ambapo mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika makusanyo ya kodi, licha ya changamoto mbalimbali katika kipindi cha mwaka uliopita 2019/20 walikusanya jumla ya shilingi bilioni 420.83 ikiwa ni ongezeko la asilimia 12 ukilinganisha na kipindi kama hiki kwa mwaka wa fedha uliopita.

Naye Afisa Msimamizi wa Kodi Mkuu James Ntalika kutoka Kitengo cha Elimu kwa Mlipakodi TRA makao makuu Dar es Salaam amesema, lengo lao ni kuweka ukaribu kati yao na wafanyabiashara ambapo zoezi hilo ni la nchi nzima.

Amesema ipo mikoa ambayo wameshaenda tayari ,kwa Arusha wameanza zoezi hilo Septemba 7, mwaka huu na litafanyika katika katika wilaya zote na vitongoji vyake na watachukua maoni kwa wafanyabiashara,kushughulikia matatizo ya wadau wao na kuwa daraja.
Afisa Msimamizi wa Kodi Mkuu, James Ntalika kutoka Kitengo cha Elimu kwa Mlipakodi TRA akiendelea kutoa elimu jijini Arusha.

Pia Afisa huyo amewataka wadau kuondokana na ile dhana kwamba TRA inatisha au kufunga maduka zikiwemo biashara nyingine na kukimbia.Zinazofanana soma hapa.

Amesema, mambo ambayo wanatolea elimu ya mlipakodi ni pamoja na utunzaji wa kumbukumbu,mauzo kwa siku,manunuzi na matumizi,hiyo itamrahisishia mlipakodi kupata kodi stahiki wakati anafanyiwa makadiriao, kuliko kukisiwa kwani atajikuta analipa kiasi ambacho si sahihi.

Amesema, changamoto kubwa waliyokutana nayo katika kuwatembelea wadau hao ni pamoja na kutokuweka sehemu zinazoonekana katika biashara zao Namba ya Utambulisho kwa Mlipakodi (TIN) na wengine wanasema kuwa zipo nyumbani ama kwenye droo na hawatunzi kumbukumbu.
Ratiba ya TRA katika kuendesha Kampeni ya Mlango kwa Mlango.



Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news