Miongoni mwa mazao ya biashara yanayoliingizia taifa fedha nyingi za kigeni ni korosho. Zao ambalo linalimwa kwa wingi katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani, Tanga na Ruvuma. Mkoa wa Mtwara unatajwa kuwa kinara wa uzalishaji zao hilo kwa mikoa yote 20 inayolima korosho nchini. Katika msimu wa 2017/2018 iliingizia nchi dola 585.1 milioni, ambazo ni sawa na shilingi 1.3 trilioni za Kitanzania, anaripoti Ahmad Mmow (Diramakini) Kanda ya Kusini.
Korosho ambazo Afrika Mashariki zililetwa na kuingizwa na Wareno katika karne ya 16 hazikuingizwa na kupandwa kwa ajili ya biashara kama ilivyo sasa. Bali kwa ajili ya kudhibiti mmomonyoko wa udongo. Lakini baadae zilifanywa kuwa zao la biashara. Hata hivyo, mikorosho ya asili haikuwa na ubora kama ilivyo mikorosho ya sasa. Tena inaelezwa kwamba kipindi hicho ilikuwa haipatwi na visumbufu wala kudhuriwa na magonjwa na wadudu waharibifu.
Hapa nchini korosho zilianza kupandwa kwa wingi baada ya vita kuu ya pili ya Dunia na kuendelea kuongezeka katika miaka 1960. Ambapo uzalishaji ulipanda na kufikia tani 145,000 mwaka 1973/1974 kutoka tani 8,000. Kiwango ambacho kilisababisha kuwa nchi ya pili kwa uzilishaji duniani. Ikitanguliwa na Msumbiji.
Hata hivyo, katika msimu wa 1986/1987 uzalishaji wa zao hilo ulishuka kwa kiasi kikubwa hadi kufikia tani 16,400. Moja ya sababu inayotajwa kusababisha hali hiyo ni kuibuka kwa ugojwa wa ubwiri unga. Lakini juhudi zilizofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Mazao ya Kilimo cha Naliendele ( TARI-Naliendele) ulipatikana ufumbuzi uliodhibiti ugonjwa huo.
Ambapo njia mbalimbali kupitia utafiti uliofanywa na kituo hicho zilipendekezwa na zilitoa matokeo chanya.
Ugunduzi wa mbegu bora zenye ukinzani dhidi ya ugonjwa huo na ugunduzi wa viwatilifu ni baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kutokanana utafiti huo.
Japokuwa kiasi cha uzalishaji kimekuwa kinabadilikabadilika, lakini kwa jumla uzalishaji umeongezeka hadi kufikia tani 313,000 katika msimu wa 2017/2018. Kiwango kinachotajwa kuwa ni kiwango cha juu kuwahi kufikiwa hapa nchini tangu zao hilo kuingia na kupandwa hapa nchini.
Kwa mujibu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) mwenendo wa uzalizhaji korosho ghafi duniani umeongezeka. Kwani hivi sasa umeongezeka kutoka tani 3,754,910 msimu wa 2014/2015 hadi kufikia tani 5,985,573 msimu wa 2018/2019. Ongezeko ambalo ni sawa na asilimia 37.
Ushahidi wa ongezeko la zao hilo ni kupanda kwa kiwango cha uzalishaji hapa nchini wa kuwa na wastani wa tani 200,000 hadi 300, 000 kwa mwaka. Huku kukiwa na mipango na mikakati ya kuongeza uzalishaji ili kufikisha tani 1,000,000 kwa mwaka ifikapo mwaka 2023/2024.
Hapa nchini mikoa inayolima korosho imeongezeka. Ni kutokanana jitihada za serikali kupitia Bodi ya Korosho kuongeza uzalishaji. Hivi sasa mikoa inayolima korosho imefikia 20 kutoka mitano ya awali. Lakini pia ongezeko la maeneo yanayolima korosho haliishii Tanzania tu, bali duniani kote. Ikielezwa kwamba nchi zinazozalisha korosho zimeongezeka kutoka 20 mwaka 2010 hadi nchi 40 mwaka 2020. Huku ikishuhudiwa kushamiri mipango na mikakati ya kuongeza uzalizhaji.
Mathalani hapa nchini, serikali kupitia Bodi ya Borosho (CBT) mwaka 2017/2018 ilianzisha mpango wa kuzalisha miche 10,000,000 kwa kipindi cha miaka mitatu. Ni dhahiri kwamba iwapo mpango huo utatekelezwa kikamilifu, bila shaka azima ya kufikisha tani 1,000,000 za korosho ghafi ifikapo 2023/2024 itafanikiwa.
Kuongeza uzalishaji kuna faida nyingi. Faida chache miongoni mwa nyingi ni nchi kujitangaza katika soko la kimataifa. Hivyo kuvutia wafanyabiashara kuja kununua korosho ghafi hapa nchini. Lakini pia kutachangia upatikanaji wa malighafi za viwanda vya ndani vya kubangua korosho. Ambavyo vitaongeza fursa za ajira kwa wananchi ambao watafanya kazi kwenye viwanda hivyo. Hasa wanawake. Ikizingatiwa kwamba viwanda vya kubangua korosho wafanyakazi wake wengi ni wanawake.
Hata hivyo pamoja na mipango hiyo mizuri ya nchi na ongezeko la korosho ghafi lakini nchi zinazonunua na kubangua kwa wingi zimeendelea kubaki kuwa mbili tu. Ambazo ni India na Vietnam. Hali ambayo inatoa picha ya kuwepo ugumu wa soko unaosababishwa na kukosa ushindani sokoni. Mathalani asilimia 74 ya tani 232681 za korosho za msimu wa 2019/2020 zilikwenda katika nchi ya India pekee.

Kwa kuangalia mwenendo huo wa soko tunabaini kwamba mwenendo wa korosho ghafi kwa soko la nje hauridhishi. Lakini pia kuna tishio jingine linalokabili soko la korosho zetu. Kwani moja ya nchi hizo zinazonunua na kubangua, Vietnam imeanza kuzalisha korosho ghafi. Huku pia nchi majirani wa Vietnam na India ambazo ni Cambodia na Indonesia zinazalisha korosho. Kwa hiyo upo uwezekano wa kutokuja kununua korosho zetu kutokana na umbali baina ya Tanzania na nchi hizo. Kwa hiyo kuendelea kutegemea soko la nje ni sawa na kutegemea anguko la soko la zao hilo.
Kwa bahati nzuri, Bodi ya Korosho imeona hatari inayokuja. Kwa hiyo haijasubiri ije ndipo ianze harakati za kukabiliana nayo. Bali imeamua ianze kuikabili kabla hali haijawa mbaya. Ndipo ilipokuja na mpango wa kupata soko mbadala. Kwa kuwa na mkakati wa mambo mawili yanayotakiwa kufanyika ili kufanikiwa mpango huo. Ambayo ni kuhakikisha korosho zinabanguliwa hapa nchini na bidhaa zinazotokana na korosho zinaanza kupata soko kubwa la ndani.
Bodi ya Korosho katika kutimiza azima yake hiyo, katika maonesho ya wakulima (Nanenane) ya mwaka 2020 ya Kanda ya Kusini yaliyofanyika Ngongo, Manispaa ya Lindi ilizindua mpango wa uhamasishaji ubanguaji na utumiaji wa bidhaa zinazotokana na korosho ambao umepewa jina la Siku ya Korosho.
Bodi ya Korosho katika kuhakikisha dhamira yake ya kupata soko mbadala inatimia imepanga katika mwaka 2020/2021 itakutana na wadau wa korosho. Wakiwemo halmashauri za wilaya, sekretarieti za mikoa, vyama vya ushirika,wabanguaji, Taasisi ya Utafiti wa Mazao ya Kilimo (TARI), taasisi za fedha na mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuandaa mapendekezo ya utekelezaji wa soko la awali la korosho ili kuwapa kipaumbele wabanguaji wa ndani. Kwani ni muhimu katika k ubaini mahitaji ya wabanguaji ndani ya nchi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa CBT, Francis Alfred amesema serikali imetangaza mpango huo kutokana na kutambua kwamba korosho zilizobanguliwa zina wigo mpana wa soko ikilinganishwa na korosho ghafi. Lakini pia uhamasishaji ulaji na ubanguaji nia yake ni kunusuru anguko la bei ya korosho ambayo imeanza kutetereka. Akitolea mfano msimu wa 2017/2018 ambao bei ya korosho ghafi ilifikia shilingi 4,128 kwa kila kilo moja. Hata hivyo bei hiyo ilishuka msimu wa 2019/2020 hadi kufikia shilingi 2,890 sawa na anguko la asilimia 30.
Amesema, hatua hizo zinachukuliwa kutokanana kutambua kwamba bei ya korosho ni motisha pekee inayoweza kuwafanya watu wawekeze kwenye sekta ya kilimo. Hasa kilimo cha korosho hapa nchini.
Kaimu mkurugenzi mkuu huyo wa CBT amesema, korosho zikibanguliwa hapa nchini kiwango cha fedha za kigeni zitaongezeka na kujitosheleza. Lakini pia kuuza korosho zinazozalishwa nchini kupitia soko la ndani litawezesha pia wakulima kupata soko la uhakika na bei nzuri.
Mtaalam wa utafiti
Maelezo ya Alfred yanaungwa mkono na Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Mazao ya Kilimo cha Naliendele (TARI-Naliendele), Dkt.Fortunatus Kapinga ambae anasema, matumizi ya mazao ya korosho hapa nchini ni madogo sana.
Akitolea mfano korosho kupewa kipaumbele kuliko mabibo, kuthamini korosho karanga ambazo kwa uzito ni wastani wa asilimia 20 hadi 25 tu ya korosho ghafi, ngozi laini ( testa) ambayo ni asilimia mbili na ganda (shells) ambazo ni asilimia 75 hadi 80 ya uzito wa korosho ghafi havihesabiwi kwenye thamani ya korosho ghafi.
Mtaalamu huyo wa utafiti wa mazao ya kilimo amesema katika kuongeza thamani ya korosho, licha ya kubangua, taasisi hiyo inafanya utafiti na kubaini njia nzuri za kuongeza thamani ya korosho kwa kutengeneza bidhaa zinazotokanana zao hilo. Kama vile siagi (cashewnut butter) na maziwa ya korosho (cashewnut milk). Ambapo utafiti wa maziwa ya korosho upo kwenye hatua ya uangalizi (shelf life). Pia imeweza kugundua na kupendekeza utengenezaji wa bidhaa za mabibo. Ikiwemo mvinyo wa mabibo (cashew wine) jamu ya mabibo (cashew jam) na sharubati ya mabibo (cashew juice).
Dkt.Kapinga amesema, kwa kula korosho binadamu wanapata viinilishe vingi ambavyo vinasaidia kuimarisha afya zao kwa kutia joto na protini nyingi zaidi kuliko hata iliyopo kwenye samaki na nyama. Lakini pia zina virutubisho vingine vingi muhimu kwa ajili ya kujenga mwili.
Amesema, watu wengi wanaona kwamba korosho ni kama karanga za kawaida. Lakini ukweli ni kwamba zina faida nyingi. Kwani zina viinilishe vingi muhimu mwilini ambavyo haviwezi kupatikana katika aina nyingine ya karanga. Lakini pia zina madini muhimu mwilini kama fosiforasi, sodiam, potasiam,magniziam, chuma, zinki, shaba na madini yanayolinda mwili na mishipa ya fahamu na hazina lehemu. Kwahiyo zinapunguza uwezekano wa kupata magojwa ya moyo.
"Korosho zinaweza kuliwa na kila mtu kuanzia watoto,wazee, wagonjwa na hata akina mama wajawazito na wanao nyonyesha. Korosho kama chakula zina matumizi mengi, ikiwamo kula moja kwa moja zikiwa nyeupe mara tu ya kubanguliwa na kumenywa, kukaangwa na kuongezwa chumvi, asali na pilipili baada ya kumenywa. Kutengeneza siagi ya kupakwa kwenye mikate, maziwa, chocolate, ice cream, biscuit na keki. Ambapo mwilini zinafanyakazi ya kuongeza joto,"Dkt.Kapinga anabainisha na kuchambua faida za korosho.

Naibu Waziri
Nae Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba licha ya kupongeza CBT anasema ili jitihada za kubangua korosho nchini ziweze kufanikiwa kunakila sababu ya wananchi kujenga mazoea ya kuthamini na kutumia bidhaa zinazotengenezwa nchini na sisi wenyewe. Akiongeza kusema kwamba tunatakiwa kuthamini na kutumia bidhaa tunazozalisha badala ya kuona fahari kuthamini na kutumia bidhaa zisizotengenezwa na sisi wenyewe.
Amesema kwa uzalishaji wa korosho ghafi uliopo ni wastani wa tani 300, 00. Unaweza kutengenzwa na kuzalisha tani 60,000 za korosho karanga (carnels) ambazo iwapo kila Mtanzania akila kilo moja ya korosho hizo soko la ndani pekee litawezesha wakulima kupata soko la uhakika.
Kuhusu hali ya ubora wa miundombinu, naibu waziri huyo anasema miundombinu ya ubanguaji korosho hapa nchini siyo ya kuridhisha. Kwani mpaka sasa kuna jumla ya viwanda 21 tu vinavyofanya kazi. Huku viwanda 12 vikiwa havifanyi kazi. Wakati viwanda vyote vya kubangua korosho vilivyopo nchini vikifanya kazi vina uwezo (Installed capacity) wa kubangua wastani wa tani 78,000 kwa mwaka.
Amesema, viwanda vinavyofanya kazi kwa sasa vina uwezo (utilized capacity) wa kubangua wastani wa tani 12,807 tu kwa mwaka. Wakati vikundi vya ubanguaji vinabangua korosho chini ya tani 100 kwa mwaka. Ingawa uwezo wa kubangua korosho zetu tunao.
Amesema, pia kuna fursa ya masoko ya kikanda kama vile Uganda, Kenya na Burundi. Na kwa Afrika ya Kaskazini kuna Misri. Lakini pia kuna nchi za Congo na Afrika ya Kusini. Pia malighafi ya kutosha ipo, vikundi vingi vinaongozwa na vyama vya msingi vya ushirika ( AMCOS) vyenye mfumo nzuri wa usimamizi kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), ardhi ipo ya kutosha, nishati, nguvu kazi na mtandao imara wa barabara na uongozi bora unaozingatia na kuheshimu utawala bora na sheria nao upo.
Amesema, vivutio vyote hivyo vinafanya kuwe na mazingira rafiki kwa wawekezaji wa ndani na nje kuja kuwekeza kwenye ubanguaji wa korosho nchini. Kwa kujenga viwanda vikubwa, kati na vidogo. Ni kutokanana mwelelekeo wa uchumi wa kati ambao tayari umefikiwa. Anabainisha kwamba, serikali inalenga ubanguaji korosho ufanywe na vikundi na mtu mmoja mmoja. Huku viwanda vikubwa na vyakati vikiwa na maeneo maalumu ya kumalizia.
CBT
Maaelezo ya Naibu Waziri Mgumba yanaungwa mkono na Kaimu Mkurugenzi wa CBT, Afred ambaye anasema nchi za India na Vietnam ambazo ndizo zinanunua na kubangua korosho ghafi zimefanikiwa baada ya kusimamia, kuzingatia na kuwekeza kwa kujali mnyororo wa thamani katika kuwekeza. Matokeo ya jitihada hizo ni nchi hizo kuweza kununua korosho nyingi na kubangua. Hivyo kuwezesha wananchi wake kupata ajira kwenye viwanda hivyo vya kubangua korosho.
Kaimu mkurugenzi huyo wa CBT anasema, mnyororo wa thamani ni muhimu sana ili kufanikiwa kufikia azima ya serikali kupitia bodi hiyo. Mnyororo wa thamani ambao unaanzia mashambani ambako udhibiti wa ubora wa korosho unaanzia. Wakulima wanatakiwa kuzingatia ubora kuanzia wakati wa palizi, kupulizia dawa za kuua wadudu, kukinga ukungu na mengi mengineyo kwa kuzingatia maelezo ya wataalamu wa kilimo ili kukinga na magonjwa yanayoweza kusababisha korosho zisiwe na ubora. Lakini pia uangalifu katika kuhifadhi korosho kabla hazijapelekwa katika maghala makuu tayari kwa kuuzwa.
Amesema, mnyororo wa thamani mchakato wake unawahusisha wadau wengi ili uweze kutoa matekeo chanya. Ndipo linapojitokeza eneo la ubanguaji ambalo moja kwa moja linahusisha viwanda.

SIDO
Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) ni miongoni mwa wadau wakubwa katika kufanikisha mnyororo wa thamani kupitia sekta ya viwanda.
Meneja wa SIDO wa Mkoa wa Lindi, Mwita Kasisi anasema ili kufanikiwa na hata kutengeneza bidhaa zinazotokanana korosho, viwanda vidogo ni muhimu sana. Kwa hiyo licha ya kupongeza mpango huo wa CBT, lakini pia aliweka wazi kwamba SIDO kama miongoni mwa wadau imejipanga vema kutimiza wajibu wake wa msingi wa kupeleka teknolojia kwa wananchi, kusimamia na kuhudumia viwanda vidogo nchini.
Kasisi anasema, SIDO inazo mashine bora ambazo bei zake ni nafuu kwa yeyote anayehitaji kuanzisha kiwanda cha kubangua korosho. Wakiwemo wakulima wenyewe. Kwani baadhi yao wana uwezo wa kununua mashine hizo kutokanana na viwango vyao vya uzalizhaji zao hilo. Kwa hiyo wasisite kwenda SIDO kununua mashine hizo za kubangua korosho ili waziongezee thamani korosho ghafi zao.
Anasema, Serikali kwa kutambua umuhimu wa viwanda vidogo na wajasirimali kwa uchumi wa nchi imekuwa ikilipatia shirika hilo fedha nyingi ili liweze kuwakopesha wajasiriamali. Wakiwamo wenye viwanda vidogo wenye uhitaji wa mitaji.
Amesema, licha ya kupeleka teknolojia na kukopesha wajasirimali wanaokidhi vigezo na sifa za kukopeshwa, lakini pia wale ambao wanahitaji viwango vikubwa vya mikopo kuliko uwezo wa shirika hilo linawasaidia na kuwaunganisha na taasisi za fedha ili wakopeshwe.
RC Mtwara
Mkoa wa Mtwara ni kinara wa uzalishaji korosho kuliko mikoa yote inayolima korosho hapa nchini. Mkuu wa mkoa huo, Gelasius Byakanwa pamoja na kuipongeza CBT kwa mkakati huo ambao utafanya kuwe na soko la ndani la uhakika alisema ili kutimiza azima hiyo ya serikali kupitia CBT kila mdau anawajibu wa kutimiza wajibu wake kikamilifu.
Amesema, wajibu huo unatakiwa kuanza kutimizwa na wakulima wa zao hilo kwakuanza kuthibiti ubora kwa kufanyia kazi maelekezo ya wataalamu wa kilimo.
Amesema wakulima wana kila sababu ya kulinda ubora ili azima ya serikali iweze kufanikiwa. Lakini pia vyama vya msingi vya ushirika navyo vina nafasi kubwa ya kufanya korosho ghafi ziwe bora au zisiwe bora. Kwa hiyo vinatakiwa kushiriki kikamilifu udhibiti ubora. Ni lazima vizingatie uhifadhi nzuri wa korosho ghafi. Kwani ni vigumu korosho zisizo bora kuweza kutengenezwa bidhaa bora.
"Wakulima kwa upande wao wana jukumu kubwa la kulinda ubora wa korosho wakati serikali ikitimiza na kutekeleza wajibu wake katika kuhakikisha wanapata bei nzuri ili wanufaike na kazi wanayofanya. Ndio sababu imekuja na mkakati huo. Kwa hiyo wanao wajibu wa kuunga mkono juhudi za serikali kwa ajili yao na uchumi wa nchi ambao unatumika kuwaletea maendeleo kwa kuboresha huduma za jamii na kutekeleza miradi ya maendeleo,"anasema..
Maelezo ya mkuu wa mkoa wa Mtwara yanatiwa nguvu na kuungwa mkono na ofisa ubora wa CBT, Joseph Merere ambae anasema ili korosho ziweze kuhimili ushandani wa soko na kutoa bidhaa bora nilazima kudhibiti ubora kwa kuzingatia hatua zote za msingi tangu zikiwa shambani hadi kufikishwa kwenye maghala makuu.
Merere amesema, kwa kutambua umuhimu wa ubora wa korosho bodi hiyo inaandaa mfumo nzuri, wa kisasa na bora kwa ajili ya taarifa za usafirishaji na mapokezi ya korosho ghafi kutoka AMCOS kwenda maghala makuu. Huku akiweka wazi kwamba korosho zitakazobainika ni chafu hazitatolewa ndani ya maghala makuu hadi kifahamike chama ambacho kimeingiza korosho hizo ili viongozi wa chama hicho wabebe gharama za kuzifanya ziwe na ubora unaohitajika.

Amesema, ubora wa korosho unaanzia kwenye palizi, kupulizia viwatilifu, kukusanya (kuvuna) kuanika na kuhifadhi. Akiweka wazi kwamba korosho zinatakiwa kuanikwa kwa muda wa siku tatu hadi nne. Lakini pia zihifadhiwe kwenye vifungashio vinavyopitisha hewa.
"Korosho zikihifadhiwa na kuanikwa vizuri zinajulikana. Zina mlio mkali zikiangukia sakafuni au zinapochezeshwa viganjani. Korosho za aina hiyo ndizo zina nafasi na uwezo wa kuhimili ushindani sokoni. Kwani ndizo zinaweza kutengenezwa bidhaa bora ambazo tunahamasisha wananchi watumie,"amesisitiza Merere.
DC Lindi
Wilaya ya Lindi ndipo zilipo ofisi za SIDO za mkoa wa Lindi., Mkuu wa wilaya hiyo, Shaib Ndemanga kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Lindi anasema upo uwezekano wa kuwa na idadi kubwa ya viwanda. Hasa vidogo iwapo kutakuwa na uhamasishaji wa uanzishaji viwanda.
Kwani baadhi ya wakulima wana uwezo mkubwa unaoweza kuwafanya wawe na uwezo wa kununua mashine za kubangua korosho toka SIDO.
Kwani wapo wakulima ambao wanavuna zaidi ya tani 40 kila mwaka. Hao wakihamasishwa wana uwezo wa kuanzisha viwanda vitakavyobangua korosho zao na za wakulima wenzao.
"Hivi karibuni nilikwenda SIDO kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Lindi, kulikuwa na hafla ya kukabidhi mashine mbili za kubangua korosho kwa chuo kikuu cha Stella Marins kilichopo Mtwara. Mashine zile mbili zinauzwa shilingi milioni hamsini na saba tu ambazo baadhi ya wakulima wanamudu kabisa kununua. Kuna wanaovuna hadi tani mia moja kwa mwaka. Hao wana uwezo wa kununua mashine zile. Na hata wenye vipato vidogo zipo mashine ambazo wanamudu kununua kulingana na uwezo wao,"Ndemanga anasisitiza.
Aidha mkuu huyo wa wilaya ya Lindi anatoa wito kwa taasisi za serikali zenye rasmali watu na ambazo zipo katika maeneo yanayolima korosho, zilime zao hilo na kuanzisha viwanda vya kubangua. Huku akizitaja baadhi ya taasisi ambazo anaamini zinauwezo huo kuwa ni Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Magereza.
Lakini pia anatoa wito kwa halmashauri kutafuta uwezekano wa fedha za mifuko ya vijana, wanawke na walemavu kupewa kipaumbele kwa kuelekezwa kwenye vikundi vya ujasiriamali vya makundi hayo vinavyotaka kuanzaisha viwanda vidogo. Pia kutenga maeneo maalum ya viwanda ambayo yatajengwa viwanda.
TANECU
Mkoa wa Mtwara unajulikana kuwa ni namba moja kwa uzalishaji wa korosho hapa nchini. Hata hivyo mkoa huo unaoundwa na wilaya za Masasi, Nanyumbu, Mtwara Mjini na Vijijini, Newala na Tandahimba unabebwa zaidi kwa uzalishaji na wilaya za Tandahimba na Newala. Wilaya hizo mbili zimeunganisha nguvu na kuunda chama kikuu kimoja cha ushirika kinachoitwa Tandahimba and Newala Co-operative Union ( TANECU).
Mwenyekiti wa chama kikuu hicho, Shaibu Haifai ambaye alizungumzia yote mawili ( ubanguaji na ulaji korosho) na udhibiti ubora anasema CBT ambayo imekuwa na ushirikiano mkubwa na vyama vikuu vya ushirika imekuja na wazo hilo wakati muafaka. Kwani soko na bei ya korosho imeanza kuyumba na kuanza kusababisha malalamiko toka kwa wakulima ambao hawajui chanzo cha kuyumba soko na kutetereka bei dhidi serikali.
Amesema kufuatia hali hiyo kulikuwa na kila sababu ya kutafutwa soko mbadala kama ambavyo serikali kupitia bodi yake ya korosho imeamua kutafuta soko mbadala kabla hali haijawa mbaya zaidi.
Amesema ili kufanikiwa azima hiyo hatua ya kwanza ni korosho kuongezewa ubora. Ambapo katika kutekeleza hilo kwa vitendo chama chake kipo kwenye mchakato wa kuanzisha kiwanda kikubwa cha kubangua korosho ili kuziongezea thamani.
Amesema, TANECU kimepanga kwenda kukopa fedha kwenye taasisi za fedha ili zitumike kujenga kiwanda hicho ambacho kitakuwa mali ya TANECU. Akiweka wazi kwamba haitakuwa mara ya kwanza kwa chama hicho kukopa fedha kutoka taasisi za fedha ili zitumike kutekelezea miradi yake ya maendeleo. Kwani iliwahi kukopa fedha ambazo zilitumika kujenga maghala makuu ya chama hicho yaliyopo wilayani Tandahimba.
Kuhusu ubora wa korosho ghafi mwenyekiti huyo amesema, ubora wa korosho uanzie katika ngazi za chini. Kwa vyama vya ushirika ni kwenye AMCOS. Kwani ndizo zinazokusanya korosho toka kwa wakulima na kuhifadhi kabla ya kupeleka katika maghala makuu. Hata hivyo changamoto iliyopo ni AMCOS nyingi kutokuwa na naghala yenye ubora. Hali inayosababishwa na uwezo mdogo wa kiuchumi. Kwani kiasi cha ushuru kinachotolewa kwa AMCOS hakimudu kujenga maghala yenye ubora. Badala yake baadhi ya vyama vinalazimika kutumia maghala yasiyo na sakafu na yanayovuja.
"Kiasi cha shilingi 50 kinachopewa vyama vya msingi hakikidhi mahitaji ingawa kimedumu kwa takribani miaka kumi na tano bila kuongezwa. Ni vema bodi kabla ya kuitisha mikutano ya wadau iwe inawaita wanufaika wa ushuru kujadiliana na kupendekeza viwango vya ushuru ambavyo bodi itapeleka kwenye mikutano ya wadau," Haifai anashauri.
Aidha, kuhusu kula na kutumia bidhaa za korosho ili kupata soko mbadala amesema, kuna haja ya bodi za mazao kuwakutanisha viongozi na watendaji wa vyama vikuu vya ushirika nchini ili kupanga jinsi ya kuzitafutia soko bidhaa za eneo moja la utawala wa vyama hivyo kwenda katika eneo jingine. Kwani bidhaa zinazotengenezwa eneo moja zina soko katika eneo ambalo bidhaa hizo haitengenezwi.
Amesema, uwezekano wa bidhaa za eneo fulani la utawala wa chama kikuu kupata soko katika eneo jingine la utawala la chama kingine ni mkubwa. Kinachohitajika ni kupanga, kuratibu na kusimamiwa vizuri na serikali.
"Vipo vyama vilivyopo katika mikoa ya Shinyanga, Morogoro na Mbeya vinatengeneza bidhaa za mpunga, hasa mchele. Kule Iringa na Njombe kuna unga wa mahindi na chai, Ruvuma kule Mbinga kuna kahawa. Bidhaa ambazo mikoa mingine kama Lindi na Mtwara hazitengenezwi. Kwa hiyo zinahitajika. Hali kadhalika kuna mikoa haizalishi korosho wala haitengenezi bidhaa za korosho. Kwahiyo mikoa hiyo ni soko zuri la bidhaa za korosho. Kinachohitajika ni uamuzi tu tutakuwa na soko kubwa la ndani lenye uhakika,"anasisitiza Haifai.
TCCIA
Katibu wa Chama cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda na Wakulima ( TCCIA) Mkoa wa Lindi, Stewart Lugongo anasema, ili kufanikiwa nia hiyo njema kuna umuhimu wa kuanza kupata majibu ya kwanini viwanda vingi vya kubangua korosho vilivyoanzishwa miaka 1980 vimeharibika na vimeshindwa kuendelea kuzalisha. Ili makosa yaliyofanyika yasijirudie na kukwamisha nia hiyo njema ya CBT.
Amesema, miongoni mwa changamoto ni usimamizi mbovu wa utekelezaji wa mipango unaofanywa na baadhi ya viongozi. Kumewa hakuna ufuatiliaji kwa wawekezaji au watu na vikundi vilivyoamua kuanzisha viwanda. Hawatembelewi na kusikilizwa changamoto zao ili wasaidiwe njia za kutatua.
"Kulikuwa na kiwanda kikimilikiwa na BUCCO nasikia hivi karibuni kipo chini ya serikali. Kuna wanawake wa umoja wa wabanguaji walianza kubangua korosho. SIDO walikuwa wanawapa ushirikiano nzuri tu. Lakini sidhani kama kuna viongozi walikuwa wanawatembelea na wanajua kinachoendelea kwa akinamama hao na shughuli za kiwanda.
"Ni kwamba akina mama hao wametawanyika na hakuna uzalishaji bidhaa unaoendelea pale. Hawana malighafi, korosho zote zilichukuliwa kwa madai kwamba lilishapatikana soko. Kwa hiyo hawakuachiwa korosho ghafi kama malighafi ya kiwanda. Sasa mambo kama hayo ni lazima yaepukwe. Wawekezaji na wajasirimali nilazima walelewe, siyo kuwaacha tu,"amesema Lugongo.
Kwa upande wake mzee Said Kalindima ambae ni mkulima wa korosho wilayani Nachingwea, wilaya ambayo inaongoza kwa uzalishaji wa korosho kuliko wilaya zote tano za mkoa wa Lindi ambazo ni Nachingwea, Liwale, Lindi, Kilwa na Ruangwa amesema kuna haja ya CBT na SIDO kushuka katika ngazi za chini za jamii kwenda kutoa elimu kuhusu mipango yake ya maendeleo.

Kuhusu kutumia, kula na hata kunywa bidhaa za korosho mkulima huyo amesema ni jambo jema Watanzania kuanza kutumia bidhaa zinazotengenezwa ndani ya nchi. Kwa hiyo mkakati na mpango wa CBT umewafungua masikio baadhi ya wananchi ambao wamesikia faida za kula korosho.
Amesema wananchi wengi wanaamini kwamba korosho ni maalumu kwa watu walio katika mataifa yaliyoendelea kiuchumi na makubwa. Tena hawajui kwamba korosho zinaweza kutengenezwa bidhaa nyingi.
Kwa kuzingatia ukweli huo anasema ni muhimu CBT ishuke na kutangaza mpango huo. Wala isitegemee uzinduzi uliofanyika wakati wa maonesho ya Nanenane kwamba ujumbe umewafikia watu wengi.

Hali kadhalika watu wengi waishio vijijini hawajui kama SIDO inakopesha fedha na inazo mashine za kubangua korosho. Lakini pia anatoa wito kwa yeyote anayejua mkakati na mpango wa CBT na yanatofanywa na SIDO awe balozi wa kufikisha kwa wenzake. Kwani kazi ya kutoa elimu na kuhamasisha isiachwe kwa SIDO na CBT peke yake.