Jeshi la Polisi limemkamata Samweli Maro Mwita, dereva wa bodaboda na mkazi wa Majohe jijini Dar es Salaam, kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya utapeli mtandaoni.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime, mtuhumiwa huyo anadaiwa kufungua akaunti katika mtandao wa Facebook akitumia jina na picha ya Hassan Mabena.Polisi wameeleza kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini mtandao wa uhalifu huo na kuwabaini wahusika wengine wanaoweza kuhusika.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo









