Serikali kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) imeweka mkazo katika kuimarisha usalama, ufanisi na ushirikiano wa mifumo ya TEHAMA katika taasisi za umma kwa mwaka wa fedha 2026/27, ikiwa ni sehemu ya mageuzi ya kidijitali yanayolenga kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Hayo yamesemwa Aprili 17,2026 bungeni Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, akiwasilisha Hotuba ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027.
Amesema kuwa e-GA itasimamia na kutathmini hali ya usalama wa mifumo na miundombinu ya TEHAMA katika taasisi 571 nchini, kwa lengo la kubaini maeneo yenye udhaifu na kutoa mapendekezo ya maboresho pamoja na kufuatilia utekelezaji wake ili kuhakikisha mifumo inafanya kazi kwa ufanisi na usalama wakati wote.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo











