Watoto 30 kati ya zaidi ya 800 wamejiunga na programu maalum ya Soccer School inayoendeshwa na GSM Foundation, yenye lengo la kukuza na kuendeleza vipaji vya soka kwa vijana.
Akizungumza na waandishi wa habari, Rais wa Klabu ya Yanga, Hersi Said amesema mafunzo hayo yatawasaidia watoto kujijengea misingi bora ya soka ikiwemo nidhamu, ujuzi na ushindani, hatua itakayowawezesha kufikia ndoto zao za kucheza katika klabu kubwa ndani na nje ya nchi.
Amesema programu hiyo ni sehemu ya jitihada za kuinua vipaji vya soka nchini na kutoa fursa kwa vijana kuonesha uwezo wao mapema.
Aidha, Hersi amesema pia kuna fursa kwa watoto wengine kujiunga na mafunzo hayo kwa kuchangia gharama nafuu, huku akibainisha kuwa vituo vya mafunzo vitafunguliwa katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwafikia vijana wengi zaidi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo























