TAKUKURU yafanikisha kurejesha viwanja vya wananchi waliodhulumiwa Dodoma

"Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma imeendelea kutekeleza majukumu yake katika kipindi cha Julai hadi Septemba, 2020 kulingana na matakwa ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007.

"Kifungu cha 7(b) cha sheria hiyo kinatutaka kuhamashisha ushiriki wa jamii katika mapambano dhidi ya rushwa na hivyo leo tunawaarifu wananchi baadhi ya kazi tulizotekeleza kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2020/2021 kwa lengo la kuwakumbusha kwamba rushwa hailipi na ni adui wa maendeleo, na kwamba Serikali yetu haivumilii vitendo vya rushwa na uonevu,"ameyasema hayo Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo kupitia taarifa iliyoonwa na Mwandishi Diramakini.

Kwanza, TAKUKURU imefanikisha kurejeshwa kwa viwanja sita vyenye thamani ya shilingi milioni 72,510,000 kwa wananchi wanyonge ambao walikuwa wamedhulumiwa haki yao hadi ofisi yetu ilipochunguza na kubaini kwamba wananchi hao watatu waliokuja kutoa taarifa kwetu ndio kwa mujibu wa taratibu waliostahili viwanja hivyo vilivyopo Dodoma.

Vilevile, tumefanikiwa kudhibiti na kuokoa jumla ya shilingi 1,273,981,100 kwa aidha kurejesha serikalini, kwenye vyama vya ushirika au kwa wananchi waliostahili ambapo kati yake shilingi 323,681,100 zinajumuisha fedha zilizolipwa wakandarasi kinyume na mikataba au bila kufanya kazi, fedha za umma zilizokusanywa bila kuwasilishwa sehemu husika.

Malipo batili kwa watumishi, fedha zilizobalishiwa matumizi kinyume cha taratibu, fidia ya ardhi kwa wananchi, madeni sugu ya viongozi na wanachama wa vyama vya akiba na mikopo (SACCOS), na mikopo umiza.

"Kati ya fedha hizo shilingi 81,631,157 ambazo zimerejeshwa na wakandarasi na watumishi wa TARURA waliolipwa bila kustahili. Hii inafanya fedha za TARURA zilizorejeshwa kuanzia Juni, 2020 kufikia shilingi 104,460,557 kati ya

shilingi 124,514,024 zinazopaswa kurejeshwa. Tunawataka wakandarasi na watumishi ambao walilipwa bila kustahili kukamilisha marejesho yao kabla ya tarehe 15 ya mwezi huu,"amesema.

Pia katika fedha hizo kuna shilingi 18,000,000 za mstaafu ambaye mwaka 2016 alilipa shilingi 23,000,000 kwa kampuni moja hapa Dodoma ili auziwe trekta, lakini hakupatiwa trekta na alipofuatilia ili arejeshewe fedha zake alikuwa anazungushwa tu. Tunatarajia kumkabidhi mstaafu huyo fedha zake mara kiasi cha shilingi 5,000,000 kilichosalia kitakaporejeshwa hivi karibuni.

Aidha, shilingi 950,300,000 ziliokolewa kwa ushirikiano na Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali baada ya kufanya uhakiki uwandani na kwenye majedwali ya fidia kwa wananchi waliotwaliwa ardhi zao kwa ajili ya kupisha mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko wa nje jijini Dodoma.


Nne, TAKUKURU Mkoa wa Dodoma imeendelea kupambana na rushwa ambapo imepokea jumla ya taarifa 482 za rushwa na makosa yahusianayo, ambapo sekta ya ardhi iliongoza kwa kulalamikiwa kwa asilimia 60, ikifuatiwa na vyama vya siasa kwa asilimia 12.

Ujenzi asilimia tano, mikopo umiza asilimia tano na polisi asilimia nne. Taarifa zisizo za rushwa zilihamishiwa taasisi au ofisi husika. "Tumekamilisha uchunguzi wa majalada 16 na kufungua mashauri 15 mahakamani. Mashauri sita yalitolewa uamuzi na Mahakama, ambapo Jamhuri imeshinda mashauri manne na kushinda mawili.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news