Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, amelaani vikali tabia ya baadhi ya viongozi wa dini kutumia mamlaka na ushawishi wao kwa waumini kama kisingizio cha kuhalalisha migogoro na migawanyiko ndani ya mataifa yao.
Leo ambaye ni Papa wa kwanza kutoka nchini Marekani, ameyasema hayo kupitia ujumbe wa kurasa nne uliotolewa kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani ya Kanisa Katoliki, yanayolenga kusisitiza umuhimu wa kulinda, kuimarisha na kudumisha amani katika jamii.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo





















