Mheshimiwa Profesa Palamagamba Kabudi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki amepata ajali leo Oktoba 14,2020 mjini Morogoro, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Loata ole Sanare,mkuu wa mkoa wa Morogoro amethibitisha kutokea ajali hiyo na kusema kuwa, mheshimiwa Kabudi ambaye pia ni mbunge mteule anaendelea na matibabu.
Waziri Kabudi amepata ajali akitokea jijini Dodoma nje kidogo ya Mji wa Morogoro akiwa safari kuelekeza kwenye ziara ya kikazi jimboni kwake Kilosa mkoani humo. Tutakujuza hatua kwa hatua....
Tags
Habari
