Ajali yaua 6 wakitokea msibani

Watu sita wamefariki dunia kutokana na ajali iliyosababishwa na gari dogo (Toyota Hardtop) kuligonga lori kwa nyuma, maeneo ya kambi ya kijeshi ya Sofa iliyopo mkoani Arusha wakati wakitoka kwenye msiba wilayani Rombo, Kilimanjaro,anaripoti Mwandishi Diramakini.
Miongoni mwa waliofariki ni Padre Sixtus Massawe ambaye ni Paroko wa Parokia ya Masakta iliyopo mjini Babati mkoani Manyara.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Salum Hamduni ameeleza kuwa, ajali hiyo imetokea majira ya saa 8:20 usiku wa kuamkia leo, huku akikitaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni uzembe wa dereva wa gari la kanisa kwani alikuwa anaendesha gari kwa mwendokasi pasipokuchukua tahadhari wakati akiwa njiani.

Amesema kuwa, waliofariki katika ajali hiyo ni wanaume watano na mwanamke mmoja na kati ya hao aliyetambulika ni mmoja tu ambaye ni Padre Sixtus Massawe.

Kamanda huyo ameongeza kuwa,gari hilo lililogongwa kwa nyuma lilikuwa limesimama katika eneo hilo baada ya kupata hitilafu ya kiufundi na miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Monduli mkoani Arusha kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Pia Kamanda huyo ameyataja majina ya majeruhi sita wa ajali kuwa ni pamoja na Marko Slaa (56), Muiraq na mkazi wa Masakta, Patrice Faustine(34), Silas Giani, Timoth Faustine, Dismas, Francis Gitayane (57) ambao wote ni wakazi wa Masakta na wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru jijini Arusha.

Post a Comment

0 Comments