Armenia, Azerbaijan kusitisha mapigano

Serikali ya Armenia na Azerbaijan zimetangaza mapema leo makubaliano ya kusitisha mapigano kuhusu Mkoa wa Nagorno-Karabakh ulioko Azerbaijan chini ya mwafaka uliotiwa saini na Urusi.
Wanajeshi wa kulinda amani wa Urusi wamepelekwa mapema leo katika mkoa ulioharibiwa kwa vita wa Nagorno-Karabakh kama sehemu ya mpango wa kusitisha mapigano ambao Rais Vladmir Putin amesema, utasafisha njia ya kupatikana suluhisho la kudumu la kisiasa kwa mgogoro wa eneo hilo.

Mpango huo, uliosainiwa na Armenia, Azerbaijan na Urusi, ulioanza kutekelezwa usiku wa manane jana umefuatia mgogoro uliowauwa maelfu ya watu, kusababisha wengi kupoteza makazi na kutishia kuitumbukiza kanda hiyo nzima katika vita.

Chini ya mkataba huo, Azerbaijan itayadhibiti maeneo yote iliyoyakamata, ukiwemo mji wa pili kwa ukubwa wa mkoa huo, Shusha, nao wanajeshi wa Kiarmenia wasalimishe udhibiti wa maeneo mengine kadhaa kati ya sasa na Desemba Mosi,mwaka huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news