Ni Ndugai tena Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Leo Novemba 10, 2020 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limemchagua Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai kuwa Spika wa Bunge la 12, baada ya kupata ushindi wa kura kwa asilimia 99.7.

Katika uchaguzi uliofanyika bungeni Dodoma, Ndugai amepigiwa kura na wabunge wateule 344 kati ya wabunge 345 na kura ya hapana ilikuwa ni moja.
Ndugai amesema kuwa Bunge la 12 litakuwa ni Bunge bora na lenye mfano wa kuigwa kuliko mabunge yoyote yale na kwamba katika Bunge hilo hakutakuwa na kambi rasmi ya upinzani Bungeni kwa kuwa hawajatimiza asilimia 12.5, kwa mujibu wa kanuni za Bunge.

Post a Comment

0 Comments