Arusha wenyeji wa michuano ya CECAFA U-20

Baraza la Michezo Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limetangaza michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 itataanza kutimua vumbi Novemba 22 , 2020 jijini Arusha, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Rais wa CECAFA ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema michuano itashirikisha nchi tisa huku nchi mbili zikishindwa kushiriki.

Karia amesema, michuano hiyo ilikuwa ifanyike Aprili, mwaka huu nchini Sudan , lakini kutokana na kuibuka kwa virusi vya Corona (COVID 19) ikabidi kuahirishwa na ndio yatafanyika mwishoni mwa wiki hii.

Rais Karia ameongeza kuwa, michuano hiyo itakuwa na vituo viwili vya Arusha na Karatu huku timu zikigawanywa kwenye makundi matatu.

Timu zitakazo shiriki ni wenyeji Tanzania, Zanzibar, Somalia, Djibouti, Kenya, Uganda, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini huku Eritrea na Rwanda ndio pekee ambao hawata shiriki katika michuano hiyo.

Post a Comment

0 Comments