Nuru mpya yaonekana chanjo ya Corona

Mkuu wa kampuni ya dawa ya nchini Marekani iitwayo Moderna, Stephen Hoge ameyakaribisha mafanikio yaliyopatikana na kusema yanaleta matumaini kwamba chanjo dhidi ya virusi vya corona (COVID-19) itasaidia kuzuia janga hilo na kurejea kwa maisha ya kawaida ndani na nje ya Marekani, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Hayo yanajiri baada ya kampuni hiyo kutangaza kuwa, uchambuzi wa awali unaashiria kwamba chanjo yake inayoendelea kufanyiwa utafiti inaweza kuzuia virusi vya COVID-19 kwa asilimia 94.5 au pengine zaidi.


Aidha, matokeo hayo yapo katika hatua muhimu ya majaribio ya maabara huku yakifanana na yale yaliyofikiwa na kampuni mbili za Pfizer na BioNTech ambazo zilitangaza kwa pamoja wiki iliyopita kuwa chanjo wanayoitengeza imepata mafanikio kwa asilimia zaidi ya 90 kwa sasa.

Umoja wa Ulaya umesema tayari umeanzisha mazungumzo na kampuni ya Moderna ili kupata shehena ya dozi milioni 160 ya chanjo hiyo baada ya kuthibithishwa rasmi.

Post a Comment

0 Comments