Babu miaka 60 kizimbani kwa tuhuma za kumbaka mjukuu

Mzee mwenye umri wa miaka 60 mkazi wa Shehia ya Finya Wilaya ya Wete amefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Kaskazini Pemba akituhumiwa kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitano, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mzee huyo anafahamika kwa jina Haroub Abdalla Hamad pia anatuhumiwa kumfanyia udhalilishaji mkubwa wa kijinsia mtoto huyo jambo ambalo ni kosa kisheria.

Kesi hiyo ilisomwa katika Mahakama ya Wilaya ya Wete chini ya Hakimu wa Mahakama hiyo, Rashid Magendo kwa kuwa Hakimu wa Mahakama ya Mkoa alikuwa nje ya Mahakama kikazi.

Imedaiwa mahakamani hapo na Mwendesha mashitaka wa Serikali, Mohammed Said Mohammed kwamba mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo tarehe isiyofahamika ya mwezi Oktoba, 2020 kati ya saa 6:30 mchana na saa 11:00 jioni huko Bahren Finya.

Amesema kwamba siku ya tukio, bila ya ridhaa yake alimbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitano (jina tunalo) ikiwa ni kinyume na kifungu cha 108 (1),(2),na kifungu cha 109 (1) cha Sheria ya Adhabu namba 6/2018 sheria za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mwendesha mashataka ametaja kosa lingine mbadala la udhalilishaji mkubwa wa kijinsia kinyume na kifungu cha 139 (1),(a) ,(2),(b) cha sheria namba 6/2018,sheria za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

“Mheshimiwa Hakimu shauri hili limekuja kwa ajili ya kutajwa, lakini kwa kuwa lilistahili kusikilizwa katika Mahakama ya Mkoa,tunaomba upange tarehe nyingine,”alishauri.

Hata hivyo mtuhumiwa huyo hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo kisheria wa kusikiliza kesi za aina hiyo na mtuhumiwa amepelekwa rumande hadi Novemba 12,mwakwa huu kesi hiyo itakapokuja kutajwa katika mahakama ya mkoa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news