Mahakama yasimamia uteketezaji wa dawa za kulevya

 Zaidi ya kilo 242.106 za dawa za kulevya zimeteketezwa katika kiwanda cha Twiga Cement kilichopo Wazo Tegeta jijini Dar es Salaam kwa mtambo maalumu kutokana na amri ya Mahakama baada ya kesi ya dawa hizo kumalizika, anaripoti Mwandishi Diramakini
Dawa hizo ni kilogramu 118.174 za heroine, kilogramu 3.932 za cocaine na kilogramu 120 za bangi ambazo watuhumiwa wake wamepatikana na hatia ya kutumikia kifungo gerezani.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Edwin Kakolaki amesema leo Novemba 12, 2020 kuwa, kwa utaratibu lazima wakati wa uteketezaji huo wa dawa za hizo lazima wawepo mashuhuda wa kushuhudia kuteketezwa kwa dawa hizo.

Amesema, shuhuda anashuhudia amri ya mahakama inafanyika na hilo wanalifanya kwa uwazi ili Watanzania wajue kesi inapokuja mahakamani na kesi kumalizika lazima vielelezo viteketezwe kwa uwazi.
 
Jaji huyo amesema dawa, hizo zinateketezwa kutokana na amri ya Mahakama baada ya kesi kufika mahakamani, kusikilizwa na kumalizika kisha kupokelewa kama kielelezo cha mahakama na baadae hutoa amri ya kuyateketeza.

Pia amesema, vielelezo vinavyopokelewa mahakamani na kesi kumalizika vinateketezwa na kwamba zile taarifa kwamba kesi zake zikiisha huwa vinarudi mitaani sio za kweli.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP ), Biswalo Mganga amesema dawa zilizoteketezwa ni kilogramu 118.174 za heroine, kilogramu 3.932 za cocaine na kilogramu 120 za bangi zilizotokana na kesi 15 mbalimbali.

DPP Mganga amesema Oktoba, 2019 waliteketeza kilogramu 10.65 za cocaine na kilogramu 226.149 za heroine zillizotokana na kesi 17.

"Kwa kipindi cha mwaka 2019  na mwaka huu, jumla ya kilogramu 345.22 za heroin zimeteketezwa na cocaine kilogramu 14.5 na bangi kilogramu 120 zikihusisha kesi 32 kwa Dar es Salaam pekee,"amesema.

Amesema, dawa za kulevya zina madhara makubwa  kwa binadamu ndio maana Serikali imekuwa ikipambana katika kutokomeza biashara na matumizi ya dawa hizo kwa lengo la kuzalisha nguvu kazi hasa kwa vijana.

DPP amesema, dawa za kulevya zinachochea watu kufanya makosa na kushindwa kufanya shughuli halali, kwamba Serikali inapambana ili nchi ibaki salama kwa kuondoa na kupunguza uhalifu.

Pia amesema, kesi iliyokuwa dawa za kulevya nyingi aina ya heroine ni iliyowahusisha raia wa Iran ambao wawili wamehukumiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kutumikia kifungo cha miaka 30 jela.

Amesema, Mahakama ilitaifisha jahazi ambalo lilihusika kusafirisha dawa hizo ambazo heroine, kilogramu 111.02.

DPP Mganga alitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa juu ya dawa hizo na kufika mahakamani ili mahakama ifikie hatua kama ya jana ya kuteketeza dawa hizo kwa faida ya Taifa na watanzania kwa ujumla.

Kwa upande wake, Kamishna wa Ukaguzi na Sayansi Jinai wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na  Dawa za Kulevya, Bertha Mamuya amesema uteketezaji wa dawa hizo ni wa utaalamu wa hali ya juu na hauna madhara kwa mtu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news