Rais Jerry Rawlings afariki akiwa na miaka 73

Rais wa zamani wa Ghana, Jerry Rawlings amefariki leo Novemba 12,2020 akiwa na umri wa miaka 73, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyoonwa na Mwandishi Diramakini kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Ghana, Nana Addo Dankwa Akufo-Addo.
Hayati Rawlings atakumbukwa kama kiongozi aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi nchini humo, mara mbili na baadaye kuleta mfumo wa demokrasia kwa taifa hilo la Afrika Magharibi.

Alimng’oa madarakani, Jenerali Fredrick Akuffo mwaka 1979 wakati huo akiwa Luteni wa Jeshi nchini humo.

Baadaye alikabidhi madaraka kwa serikali ya kidemokrasia, lakini miaka miwili akaongoza mapinduzi ya pili ya kijeshi, akiituhutumu serikali hiyo kwa ufisadi na uongozi dhaifu ambao ulishindwa kutoa huduma bora kwa wananchi.
Kati ya mwa 1981 na 1993, Rawlings alitawala akiwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Pamoja wa Kijeshi na Kiraia. 

Aidha, mwaka 1992, alichaguliwa rais chini ya katiba mpya ya Ghana, na kuhudumu kwa mihula miwili, kabla ya kustaafu na kumwachia uongozi mrithi wake, Rais John Kufuor, mwaka wa 2001. Viongozi, wananchi kutoka kila kona ya Dunia wameelezea kushtushwa na kifo cha kiongozi huyo mstaafu.

Post a Comment

0 Comments