Mwanaume adaiwa kufufuka akiwa mochwari Kenya

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Peter Kiplangat  kutoka Kaunti ya Kericho nchini Kenya amewashangaza wengi na kuibua gumzo mitandaoni baada ya kudaiwa kufufuka akiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti (mochwari) saa chache baada ya kupelekwa kwenye chumba hicho.
Kwa mujibu wa mjomba wake, Denis Langat, Peter Kiplangat alipelekwa hospitalini Jumanne ya Novemba 25,2020 asubuhi baada ya kupoteza fahamu akiwa nyumbani, lakini akathibitishwa kufa alipofikishwa hospitalini hapo.

Langat amedai kuwa, Peter alishituka na kupiga mayowe baada ya mhudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti kupasua sehemu ya paja.

Huo ni mojawapo ya mchakato ambao hufanywa kama njia moja ya kuuhifadhi mwili unapowekwa kwenye chumba cha maiti, ndipo mhudumu huyo alipokimbia na kumuita daktari.

Akizungumza na waandishi wa habari katika kaunti ya Kericho, daktari mkuu wa Kapkat, Gilbert Cheruiyot amesema kuwa,Denis Langat alifikishwa hospitalini akiwa amepoteza ufahamu, lakini ndugu zake walipoona kuwa wauguzi wanachukua muda kuwashughulikia, wakampeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Post a Comment

0 Comments